Unakumbuka visa vya wamba hawa lodilofa madenge ndumilakuwili cmrd kipepe dr love pimbi zena & betina

Unakumbuka visa vya wamba hawa lodilofa madenge ndumilakuwili cmrd kipepe dr love pimbi zena & betina

Hawa wamba ndio walikuwa wakileta burdani sana enzi hizo hamna Facebook Instagram Tiktok wala Youtube.

Unavyokaribia mwanzo wa mwaka mnasubiri kwa hamu toleo la jarida jipya lililobeba katuni zilizojaa visa na vitimbi vya hao wamba. Mwanzo wa mwaka kama hivi jarida linakuwa tayari limeshatoka na sasa waja mna-enjoy tu mwaka mpya na mambo mapya.

Hapo unakuta Dr love pimbi huyu alikuwa kifupi kama stuli lakini mara zote unakuta harakati zake ni kufukuzia vimwana wasio saizi yake hasa akimfukuzia huyu tandam anaitwa Zena, Zena yeye ni tandam alikuwa na bifu zisizoisha na kimbaumbau Betina na mititi yao isiyoisha kila uchao kiasi cha kushikana mwilini, Betina alikuwa mkorofi na mjuvi wa kutupa ndonga wakikutana ilikuwa lazima Zena akae.

Lodilofa, ni baba mwenye bonge la mkitambi wake akimiliki kigari chake ki-bettle na mara nyingi hupendea kuvaa shati moja kuubwa la vipande vitatu linalomeza kitambi chake chote. Huyu bwana kuna siku kapigwa mkono na trafiki akaambiwa awashe taa za gari yake. Yeye akaishia kumjibu yule trafiki "lete giza"🤣 bila kumsahau madenge akiwa na vitendeakazi vyake rungu na manati yake.

Kulikuwa na mechi kali sana kati ya bush starz wakiongozwa na mshambuliaji wao kipenzi mapung'o wakicheza na wenzao mabon town🤣Hizi mechi zilikuwa na visa vingi sana vya kuchekesha.

Ooh....Time flies!

RIP Maestro John Kaduma na wote waliotutangulia mbele za haki
Ilikua kulikosa gazette la Sani ni kama kukosa mbingu, unasoma unamuazimisha Ndugu Jamaa na marafiki zako, likirudi unalisoma tena!
 
Ilikua kulikosa gazette la Sani ni kama kukosa mbingu, unasoma unamuazimisha Ndugu Jamaa na marafiki zako, likirudi unalisoma tena!
kabisa aisee lilikuwa halichoshi ukimaliza kusoma unalihifadhi ulisome kwa siku zijazo. akija mgeni unamtolea asome🤣muda unakimbia sana.
 
kabisa aisee lilikuwa halichoshi ukimaliza kusoma unalihifadhi kusoma siu zijazo. akija mgeni unamtolea asome🤣muda unakimbia sana.
Jamaa anasimulia Hadi na wewe unajikuta uko live, yaani yalikua kama matukio halisi kabisa.

Sasa kuna wale Jamaa wa mtaani, anawakusanya kijiweni na yeye anaanza sasa kusimulia, hahahahahha na chumvi Kibao. Ole wako ukutane na msimuliaji awe mchaga.
 
Kuna huyu mjomba ndumila alikua mwizi sana afu ana rafiki yake sokomoko mlevi sana, dah aisee umetukumbusha miaka ya 2005 afu kulikua na mjomba nchumali, ukitoka hapo kulikua na simulizi ya mzee OLE na OBI na demu mmoja Alikua anaitwa Linda na tajari mmoja alikua anaitwa MAYUKU
 
Bush Stars kabla ya mechi lazima wafanye tambiko. Utakuta jamaa wako kwenye sufuria kubwa kama chini kuna moto kama vile wanapikwa. Kuna mechi walikipiga na Man U ya kina Giggs, Scholes, Beckham na wengine... kipindi cha pili akaingia mzee Meko aliyekuwa ametoka South Africa. Mzee Meko ndo aliyeifungia Bush Stars na kushinda hiyo mechi dhidi ya Man U. Kwenye pitch majamaa yanatukanana tu.
 
Mchoraji Chris Katembo, mtunzi Ibra Radi Washokera. Unakutana na riwaya za kusisimua kama Msako wa Mr.X, Msako wa Hayawani na Eddie Ganzel. Huko unakutana na watabe kama kina Mark Steven Chenje. Ilianza Sani baadae wakaja Bongo. The return of James Akeke na Fortunatus Ndila alikua akijiita 4T Ndila
 
Back
Top Bottom