Unakumbuka wapi ukisikia majina haya?

Unakumbuka wapi ukisikia majina haya?

Amalinze

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2012
Posts
6,780
Reaction score
5,305
Habari wanabodi,

Unakumbuka nini ukisikia majina haya chini? Kipi kinakuja kichwani mwako endapo ukiona moja ya majina haya?

-Urafiki Club
-Arnatouglou
-Summit Kilimanjaro Hotel
-Vijana Social Hall
-Bahama Mama
-Imasco Centre
-Silent inn Club
-Lango la jiji
-Hotel 92
-Mbowe Club
-Magoti
-Mambo Club
-Pub Alberto
-La Prima
-Tazara Club
-Lang'ata
-Sugar Ray
-Mambo Club
-La Doci Vita
-New Chox
-Empress
-Empire
-Drive Inn
-Avalon

 
Naanza na Silent Inn tukiita sailent kila Jumamosi tulikwenda kuangalia utamaduni muungano.na kila.jumatano tulIkwenda kuangalia kikundi cha ngoma JWTZ wenyewe tuliita utamaduni Komba (RIP) hizo tano za mwisho nilikuwa sio shabiki sana maana sinema nzuri zote zilikuwa X na umri ulikuwa hauniruhusu
 
Nikisikia La prima nakumbua wazee sugu,wazee wa sauti ya umeme,ES Field Marshal.
 
Kilimanjaro hotel kwenye pool side kulikuwa na disco la Mawingu ( Boombastic sound ) with Dj Bonny Luv on the one and two.

Empire Cinema iliyokuwa azikiwe pale, Mzee alitupeleka kucheck film ya Disco Dancer ya Mithun Chakrabot kwa mara ya kwanza.
 
Zaidi ya kukumbuka kituo tu cha mwisho wa gari drive inn
labda nimuulize huyu msichana wa zamani(mama)
 
Pub Alberto Pande za moshi town, disco kipindi hicho tunasoma ilikuwa kila weekend
 
Kitambo sana Mbowe Club=Billcanas, klabu nyingi na mahoteli wamebadilisha jina sijui uwekezaji au lah anyway I love my motherland country Tz.
 
Zaidi ya kukumbuka kituo tu cha mwisho wa gari drive inn
labda nimuulize huyu msichana wa zamani(mama)

Muulize tu,Drive Inn ilikuwa ni noma kipindi hiko....Makondakta wanahita hicho Kituo "DRY"
 
Back
Top Bottom