Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasiokuwa na Seat (wanasimama)

Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasiokuwa na Seat (wanasimama)

VIP kibongo bongo bado sana, ndio tunajifunza tuseme ukweli tu... Labda miaka michache ijayo tutafika

Sasa hivi sio ajabu kukuta gari ni VVIP lakini choo kibovu, AC ya magumashi, mwendo wa dereva ni kanyaga twende babaakee, movie zilezile kila siku za mkojani, Ringo, Nagwa... Customer care mbovu, usalama wa mizigo muda mwingine mdogo kwa hiyo ni vuruguvurugu

Kuna bus (Sitalitaja) nilipanda kwenda mkoani nikajutia kutoa hela yangu kwamba nimepanda VIP.
Kama umeshindwa kulitaja basi hukuwa na haja ya kuchangia,JF tunatumia majina bandia,unaogopa nini kutaja kama sio UMBEA na UNAFIKI??
 
Hao wamasai ni kero hata kwenye daladala
Sina hamu niliwahi tupa viatu na soksi nilivyokua nimevaa🙌

Nimekaa, konda kapakia abiria njiani wamasai,akaja kuweka kindoo kati pale kawapanga hao wamasai..
Wananukaa🙌
Nikaamua kufungua dirisha na kulala...
Baada ya masaa mawili nashtuka najihisi mbichi miguuni ,sa nikawa najiuliza nimeloa na nn?
lahaula,kumbe yule mama alikuwa anatema mate pale chini anatema kwenye miguu yangu...
We mbona nilianzisha fujoo,konda kasimamisha gari, akamhamisha pale ...
Nikavua viatu vyangu na soksi nikavitupa ,uzuri Huwa nasafiri na viatu vya ziada!
Nikamwambia konda nataka maji akanipa ya chupa kubwa ikabidi wanisubiri ninawe miguu
Shenzi sana Hawa watu
 
Njia ya kwenda toilet inafungwa
Wanaosimama wanaegamia siti bus likiyumba unaangukiwa uliyekaa
Wanaegamia siti makalio yakuwa usawa wa kichwa cha abiria aliyekaa unasikia kiharufu kizito kinasambaa puani
Itatuchukua karne kadhaa kuelimika
Ana kunyea upepo[emoji1787][emoji1787]
 
Bus za Abood,New Force,alsaidy hizo zinaongoza kwa kusimamisha abiria .
Basi ambalo lina wafanyakazi wake wanafanya kazi kwa uweledi ni la kampuni ya ABC,jamaa wako vizuri sana kwenye issue ya kuhudumia abiria na hawasimamishi pia huduma ya chakula uwa ni dakika 20 pia abiria ukizidiwa njiani unasikilizwa na kuhudimiwa sio Newforce lenyewe linakimbia tu bila kujali abiria wake kisa liwe la kwanza.
 
Sina hamu niliwahi tupa viatu na soksi nilivyokua nimevaa🙌

Nimekaa, konda kapakia abiria njiani wamasai,akaja kuweka kindoo kati pale kawapanga hao wamasai..
Wananukaa🙌
Nikaamua kufungua dirisha na kulala...
Baadae ya masaa mawili nashtuka najihisi mbichi miguuni ,sa nikawa najiuliza nimeloa na nn?
lahaula,kumbe yule mama alikuwa anatema mate pale chini anatema kwenye miguu yangu...
We mbona nilianzisha fujoo,konda kasimamisha gari, akamhamisha pale ...
Nikavua viatu vyangu na soksi nikavitupa ,uzuri Huwa nasafiri na viatu vya ziada!
Nikamwambia konda nataka maji akanipa ya chupa kubwa ikabidi wanisubiri ninawe miguu
Shenzi sana Hawa watu
Pole sana ndg!
Niliwahi kushuka daladala kwa harufu ya hawa watu.
Hawana ustarabu kabisa.
 
Nilipanda Second class basi La ABC kwenda Mbeya

Ilikua poa sana
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimechekaa had baas. Huwa nawahurumia mnoo wanao simama. Uwiiiih
 
Unakuta BUS limeandikwa VIP/VVIP lakini likifika mahali linapandisha abiria wasio na siti

Kuanzia Ally stars BUS wanaoisifia , katarama BUS na Bus zingine nyingi hali hii inafanyia abiria wake.

Unakuta umepanda bus kila abiria amekaa katika seat yake ikifika mahali Bus linaruhusu kupakiza abiria wengine wanaanza kusimama pembeni ya seats za abiria wengine wanakaa katika njia za kupita.

Nini maana ya Bus kuipa Hadhi ya VIP/VVIP?

Wamiliki wa Bus suala hili mnalifahamu?

- Ni bus gani haina tabia hizi?
Mkuu unavyo sema ni kweri kabisa hata mm hua na kwazika sana,lakini nimehi kua na demu konda nili muuliza hilo swali,akasema hao wanao simama ni posho zao wanajilipa.

Madereva na mafundi,wanao safiri na gari na wale wakaguzi wa njiani na pesa ya trafic ila konda ndiyo ana wagawia wenzake wakipo trafic.
 
Back
Top Bottom