Unakwepaje Vyakula hivi

Unakwepaje Vyakula hivi

Kibongo bongo si unajua mapishi yetu ndio hayo hayo, labda itokee tu mapishi mwenye exposure kidogo ya ubunifu wa chakula au migahawa ya watu wa nje at least utabadilisha lakini nje ya hapo hata uende mgahawa gani TZ ilimradi hawana hivyo vitu viwili hapo juu basi menu ni ile ile...Hivyo wengi ubunifu ni ziro, Kuna maharage ukipikiwa Sasa hivi na mtu anayejua utajiuliza ulikuwa wapi Miaka yote hiyo...Nje ya nilivyosema hapo labda ule mchanga na HCl.
 
Uko kama mimi mkuu kuna muda nakua sina hamu ya kula options zile zile! tatizo muda wa kuviandaa na mamsap yuko kazini pia, sometimes natamani uji wa unga wa ngano nzima zile, karanga za kuchemshwa, viazi vitamu vya kuchemshwa unashushia maziwa mgando.

Watoto wangu utaskia daddy i want pizza, ya nyokwee! I buy dho 😂
 

Attachments

  • 1724915704273.jpg
    1724915704273.jpg
    235.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom