Unalipi la kusema juu ya mtandao wa YAS

Unalipi la kusema juu ya mtandao wa YAS

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Ndugu zangu siku za karibuni mliifahamu kama kampuni ya TIGO sasa imekuwa YAS una lipi la kusema juu ya mabadiliko haya

Hii imekaaje tangu ilipobadilishwa na kuitwa YAS huku huduma ya fedha ikiitwa MIXX by YAS badala ya TIGO PESA??

Je tutegemee mafanikio makubwa ama kifo cha mende??
 
Tigo gawio hawajabadilisha, meseji zinakuja umepokea tigo gawio na sio yass gawio.
 
Ndugu zangu siku za karibuni mliifahamu kama kampuni ya TIGO sasa imekuwa YAS una lipi la kusema juu ya mabadiliko haya

Hii imekaaje tangu ilipobadilishwa na kuitwa YAS huku huduma ya fedha ikiitwa MIXX by YAS badala ya TIGO PESA??

Je tutegemee mafanikio makubwa ama kifo cha mende??
1: Promo kubwa sana mtaani.
2: Kelele zakutosha ili muitambue vzr.
3: downtime za huduma zao zimeongezeka km zilivyo kelele zakulitangaza.
4: wanatamba wao ni baba lao lkn huduma zao haziendani na matangazo yao,watu wapo 5G lkn hio 4G kuna maeneo hakuna hio huduma ingawa kifaa ni 5G.
Ndio nilioyaona mimi
 
Nimefanya transaction ya 30K pesa haikufika na ktk balance yangu wamekata sielewi kwa nini mpaka sasa hawajarudisha hiyo 30K .Nimetumia App yao sasa sielewi watarudisha au ndio washakula SIJUI.
 
Screenshot_20241226-104448.jpg
 
Tuwape muda. Hakuna jambo zuri linalokuja ghafla, kubadilisha jina kunaendana na mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma bora na maboresho mbalimbali. Natarajia kuiona Yas kama mtandao bora baada ya mwaka mmoja.
 
Kifupi... Sitamani kabisa kutumia hili neno YAS ila sina namna... 🥲
 
Attachments

  • Screenshot_20241226-104733.jpg
    Screenshot_20241226-104733.jpg
    220.2 KB · Views: 7
  • 1735199618981.jpg
    1735199618981.jpg
    589.8 KB · Views: 6
Nimefanya transaction ya 30K pesa haikufika na ktk balance yangu wamekata sielewi kwa nini mpaka sasa hawajarudisha hiyo 30K .Nimetumia App yao sasa sielewi watarudisha au ndio washakula SIJUI.
Jambo hili nami lilinikuta. Nimeenda kutoa pesa kwa wakala, kwangù pesa imekwenda kwa wakala lakini sijapata sms na wakala hajapokea sms. Nikawapigia hao YAS lakini wakanijibù mtandao Tigo pesa ukò chini kwa hivyo nimwambie wakala atazame salio Lake. Wakala anasema yeye haoni pesa na akiwapigia Hao Yas hawapokei simu basi nikakubali kupokea hasara lakini nimeamua kutofanya muamala wa aina yoyote kwenye mtandao wao.
 
Tuwape muda. Hakuna jambo zuri linalokuja ghafla, kubadilisha jina kunaendana na mabadiliko makubwa ya utoaji wa huduma bora na maboresho mbalimbali. Natarajia kuiona Yas kama mtandao bora baada ya mwaka mmoja.
Buzz/Bazz,mobitel,tigo na sasa yas almost 20yrs unataka kumpatia muda gani,it’s either nimitambo mwenye Mali hawekezi or watu walionao hawana uzoefu wa wanachofanya
 
Back
Top Bottom