Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Umezaliwa humfahamu baba yako mzazi. Mama yako anakwambia babaako alishakufa. Anakutajia jina ambalo silo unalotumia shuleni. Unaanza kujiita ubin kwa hilo jina.
Baada ya miaka kadhaa,
mama yako anakutambulisha kwa mtu mwingine kuwa ndiye baba yako. Tena yuko hai. Na jina sio lile alilokutajia.
Unaanza kuuliza maswali imekuwaje. Mama yako wala huyo baba hawakupi majibu yanayokuridhisha. Unahisi kuna kitu hakiko sawa.
Baada ya miaka kupita, mama yako anakutajia jina la mtu mwingine tena na kukuonesha picha kuwa huyo ndiye baba yako. Anakupa namba. Unajaribu kupiga hiyo namba haipokelewi. Unaamua kuifuta.
Baadae rafiki wa huyo baba anakwambia kuwa; huyo baba yako hayuko tayari kukukubali. Na anauliza kwanini mama yako hakumwambia mapema. Unaamua kupotezea na kuendelea na maisha yako.
Swali ni je, utamchukuliaje huyo mama yako, Ambaye hayuko tayari kusema chochote kila unapomuuliza?