Unamfahamu msimamizi wa Mirathi?

Marichris

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
571
Reaction score
509
Kwa kuanza tu ni kwamba, msimamizi wa mirathi ni mtu yeyote aliyeteuliwa na marehemu kwenye wosia kuwa msimamizi wa mirathi baada ya kifo cha Marehemu, au mtu yeyeto aliyeteuliwa katika kikao cha ukoo kuwa msimamizi wa mirathi. Mtu yeyote ambae ni msimamizi wa mirathi kwa namna hizo mbili zilizoelezwa hapo juu,

Anapaswa kufungua mirathi mahakamani na kupewa ruhusa ya kutambua, kukusanya, na kugawa Mali za marehemu kwa warithi.

Pia msimamizi wa mirathi anapaswa kulipa madeni ya marehemu Kama yapo na kutoa taarifa za mwisho kwa mahakama za namna alivyoshughulikia Mali za marehemu.

Msimamizi wa mirathi hapaswi kutumia Mali za marehemu vibaya kwani anaweza kushtakiwa kwa madai au jinai...

Asanteni Wakuu.
 
Vizuri!

Vipi mkuu unajiandaa kusimamia mirathi ya mtu nini?
 
Kama warithi hatumkubali Huyo msimamizi na kikao cha ukoo wanamtaka itakuaje?
 
Vipi ela inatakiwa upate baada ya mda gani? Ambazo zikikuwa kwenye account ya marehemu na kuenda mahakami,
 
Vipi ikitokea marehemu hakuacha maandishi Ila alitamka mwenyewe kuwa akifariki mtu Fulani arithi Mali yake inakubalika?
Hapana mkuu, Mimi ni Mwanasheria na Wakili wa Mahakama Kuu pia
 
Ahsante Wakili. Je, kama marehemu alizaa mtoto nje ya ndoa na ndoa yake ilikua ya kikristo mtoto anapewa nini kwenye urithi?
 
Naomba kuuliza pia kwa mfano, marehemu alikuwa ni mtumishi wa umma, baada ya kufariki mirathi haikushughulikiwa kutokana na sababu mbalimbali, baada ya miaka 25, watoto wanahitaji mirathi ya baba yako ikiwemo suala la kiinua mgongo cha marehemu kutoka serikalini, je mirathi hiyo ina expire au bado ipo tu wakianza kushughulikia wataipata?
 
Mada nzuri;
Kwenye kuamdika wosia unaweza kumchagua mtoto moja wapo wa kumzaa asimamie mirathi wakati mke yupo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…