Kwa kuanza tu ni kwamba, msimamizi wa mirathi ni mtu yeyote aliyeteuliwa na marehemu kwenye wosia kuwa msimamizi wa mirathi baada ya kifo cha Marehemu, au mtu yeyeto aliyeteuliwa katika kikao cha ukoo kuwa msimamizi wa mirathi. Mtu yeyote ambae ni msimamizi wa mirathi kwa namna hizo mbili zilizoelezwa hapo juu,
Anapaswa kufungua mirathi mahakamani na kupewa ruhusa ya kutambua, kukusanya, na kugawa Mali za marehemu kwa warithi.
Pia msimamizi wa mirathi anapaswa kulipa madeni ya marehemu Kama yapo na kutoa taarifa za mwisho kwa mahakama za namna alivyoshughulikia Mali za marehemu.
Msimamizi wa mirathi hapaswi kutumia Mali za marehemu vibaya kwani anaweza kushtakiwa kwa madai au jinai...
Asanteni Wakuu.