Unamfanyia nini rafiki ,anayekujaza upigwe Kama yeye alivyopigwa na wahuni

strategist22

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2017
Posts
655
Reaction score
599
Leo nimekuwa na furaha baada ya kukutana na rafiki yangu wa shule , A level . Yeye alinitangulia darasa moja,alinipokea shule tukawa marafiki sana.

Alinitangulia pia kufika mjini , chuo UDSM mkopo mia ,akalizwa na wajanja wa mjini hapa. Ni mambo haya ya biashara za mitandaoni ,hakujua vizuri mambo yanavyoenda alitosheka na stori zao kuwa ukijiunga tu utaanza kupokea mapesa mengi mengi,utaenda marekani ,utanunua nyumba na gari mwaka huu haushi!!

Jamaa alinijuza kuwa kuna dili amepata ,baada ya muda kidogo itakuwa ni hadithi nyingine.Nilitaka kujua ni dili gani hilo,alinijuza ni kuwa anajihusisha na biashara za mitandaoni ,kuna kampuni kawekeza hela yake ya mkopo huko anasubiri mavuno tu. Sikuwa najua sana mambo hayo ,bado nilikuwa kidato cha sita.

Baada ya kumaliza 6 nilipata kazi mashambani huko ndanindani ,jamaa akawa ananisisitiza nipambane nikipata laki tano na 70 atanifanyia mpango wa kuniunganisha na kampuni hiyo ,na mimi nipate mapesa hayo.

Muda wa chuo ulipofika nikarudi kujiandaa,jamaa kila siku anasisitiza tuma hiyo pesa nikuunge ,nilimuuliza nikiweka laki tano hiyo ndakuwa naingiza shingapi faida ,nikaambiwa kila mwezi ndavuta laki nane.

Nilimshirikisha kaka,akasema achana nao utapeli huo ,nikamwambia jamaa kuwa nimepata matatizo pesa haitatosha .Ghafla alipaniki "oooh mimi nataka kukusaidia ,wewe usaidiki,mwenzako na nyumba saivi na gari ya kutembelea na biashara mjini hapa" Akanitumia picha ya nyumba ,maduka,na brevis yake. Alinishawishi sana nijiunge na kampuni hiyo ,nikawa na mwambia siko vizuri kiuchumi, sikuwa na mkopo.

Huyu jamaa hakutaka niende kwake anaposema amejenga au tuonane live,kila siku nikobize niko Uganda mara Kenya. Tulipotezeana ,nimekutana nae leo,kachoka hana matumaini ,basi nikamuuliza "boss vipi mbona mnyonge sana,gari umeacha wapi mentor wangu"

Aliniangalia kwa huzuni "sijawahi kuwa na gari "alinijibu akiwa kainamisha kichwa. Tulipiga sana stori za mafanikio yake hewa,jinsi alivyokuwa analazimishwa kutafuta watuwengine ili na yeye apate kitu . Ndipo hapo akataka kuniingiza na mimi kwa matapeli hao.

Watu kama hawa wapo,anajua kabisa yeye kapigwa anakushawishi na wewe ili upigwe ,huko kwenu mnawafanyia nini hawa marafiki wakuda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa si entertain marafiki wa kishenzi shenzi kama hao.
 
Back
Top Bottom