Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Unamkumbuka Crush wako wa utotoni? That was real and only unconditional love you will ever experience

Usiku umeangalia zako movie ya Titanic, halafu asubuhi unaingia zako darasa la sita B dawati la pembeni yako ndio amekaa crush wako, yaani unatamani darasa lizame baharini halafu wewe umuokuoe crush wako kwenye maji yenye mabarafu.
Utoto raha sanaaaaaa.
 
Dah! Kitambo anaitwa Nuru enzi hzo Azimio p/s aliuteka sana moyo bila kumuona yeye siku haishi vizuri
 
Nimegundua kuna feeling za love katika umri mdogo sana tofauti na tunavyochukulia kwa sasa lakini hali kama hizo wengi tulipita na watoto wanapitia pia

Ni wakati ambao unakuwa na upendo halisi kama love ingekuwa iko real kwa kiasi kile maisha yangekuwa ya kuvutia sana
Tunapokuja kuingia kwenye mahusiano halisi tunagundua maisha ni tofauti sana
Mambo siyo kama tulivyodhani

Unakutana na stress za mapenzi na maisha na kama hauna pesa uliyempendaga anakuwa shemeji anakuona siyo wa hadhi yake
 
Crush wangu wa utotoni ndio mume wangu
Wooow...! Hebu tupe stori kidogo mkuu, mlikua mnasoma wote? Mkaanza ma love tokea mkiwa wadogo? I hope unainjoi sana ndoa, maana ni wachache sana wanaopata bahati ya kuoa au kuolewa na crushes wao
 
Wooow...! Hebu tupe stori kidogo mkuu, mlikua mnasoma wote? Mkaanza ma love tokea mkiwa wadogo? I hope unainjoi sana ndoa, maana ni wachache sana wanaopata bahati ya kuoa au kuolewa na crushes wao
Hahahaaaa story siku ingine.
 
Asikwambie mtu, yule crush wa utotoni hasa mara nyingi inakua shule ya msingi ni mapenzi ambayo yanavuruga sana hasa ukizingatia mara nyingi mtu mabae unampenda anakua hana ata habari au aanajua unampenda ila hana habari na wewe yuko busy na yeye na crush wake.

Nakumbuka nilipokua darasa wa tano ndo nilikua na crush huyo then kwao alikua kuna duka, bas kama siku sijaenda shule na sijamuina ni lazima nitoke nikamuone hata kama sikua na nia ya kununua kitu, bahati mabaya ilikua ni kijijini kwao hadi ufike unapita kwenye mapoli ila ilikua niko radhi, nakumbuka kuna siku nyingine nakwenda dukani usiku ili nimuone lakini nikitifika unakuta hayuko dukani unakuta mama yake au ndugu zake wengine, ila hata nikisia sauti yake tu huko ndani basi nakua na furaha.

Sikuwahi kumueleza kua nampenda mana nilikosa lakusema nilipokua karibu yake, now ameolewa na hatuna mawasiliano ila mpaka sasa sijawai kuona ile hali tena.

Hakika yale yalikua true unconditional love.
Dah crush wangu nilisoma nae primary ,wote tulijua tunapendana ila utoto mwingi et tulikuja kuchapana nshamaliza chuo ,sio mbaya ndoto yangu imetimia japo siwezi kumuoa
 
Mkuu yale mapenzi ni mapenzi ya kipekee sana, bahati mbaya wengi wa macrush wale huwa ni ngumu kua ano
Kweli kabisa hujakosea Mwana!!! Daa!! Nilikuwa nako! bana kanaitwa Josephina Shana kabinti ka Daktari wa kijiji, Hukooo Tarime sehemu moja inaitwa Kibumaye, hakika Jose ulinikaa moyoni bwana wee! uko wapi Baby!!! nilikapenda hako ni hakuna tena kijiji kizima!!

Moyoni mwangu kalikuwa kazuri sana kwa hali na Mali hata iweje nilikapenda Mno nikafa kasoro kuoza, kiasi hata kangefanikiwa kunizaba vibao nisinge mudu kujibu zaidi ningekaangalia tu kujikuna !!! nakusamehe kwa dhati ya moyo!

Yaani nilikuwa nikikaona tu hivi wajameni Mwili unakufa ganzi kabisaa!!! sisemi kitu kwake nilioza nikafa hai!! hapo ni hkn dawa jamani Mapenzi yapo wala si dawa!! Mbaya zaidi Mama yake mzazi alinipenda Mnoooo!!! alikuwa ni Nurse pale kijijini walifanana!!

But by then kuongea sijui!! kutongoza sijui!! Kuanzishaa swaga sijui !! hata kangenipa nisingejua niifanyeje wajameni!!! ila kakinisemesha kidoogo tu! daaa!! bwanawee siku hiyo raha yake haisemeki njia nzima mtu akiniona anajua nina furaha!

siku hiyo nita cheka na kufurahi njia nzima ka bwege hapo mtu yeyote niombe msaada uone nakupa kabisaa!! na siku hiyo yaani kulala ni vizuri mno!! ajabu sasa drsni mie nilikuwa dororooo!!

Lkn Jose wajameni Mwee!! kalinipita mbali mnooo!! kalikuwa kana ongoza kimasomo, Mwandiko, hesabu, kuimba mwee!! kanashika number one!! hakika kaliheshimika shule nzima!! acha Darsani tu!

Ule mpango wa kujipanga kimashindano team mbili, mnakimbia team moja huku na nyingine huku kwa kushika kijiti basi kalikuwa kanakimbia hako kuliko wote kakaitwa Rocket , hapo ndo kabisaa nikazidi kuoza!!

ile tunaanza mishe mishe za kujipanga nilikuwa najitahidi kupenya niwe na jose team moja!! nilikuwa naona raha mno! japo sikusemaga! wala hakakujua kabisaa! Daa!! Mapenzi bana!! yanaanzia Mbali sana wajameni pyuu!!

Mpaka leo Jose nampenda mnooo yani!! ila sijui yuko wapi anae jua jamani anisaidie!! sababu tu mie ni mkweli nitajua uongo na ukweli!! nikimpata haijalishi ameolewa au haja olewa mimi na yeye!! yeye na mimi walipo hama kijijni sijawahi onana nae tena!!

kwa mara ya mwisho nilisikia yuko Bwasi kijijini ni Mwalimu!! awe hai awe mfu namtaka Jose! Mapenzi yangu kwake hayakuishia palepale tu yako hai mpaka leo na kesho pia !!

Lkn maajabu sasa kabinti hata mpango na Mimi hakakuwa nao Kabisaa!! drsani nilikuwa Mjinga pyuu!! hata kusoma sikujua!! ila kuandika ndo ulikuwa hunitoi!! Nilishangaa kusikia kaka yake alikuwa Polisi Mkubwa tu kafariki juzi juzi tu hapa!!
 
Back
Top Bottom