Mkuu yale mapenzi ni mapenzi ya kipekee sana, bahati mbaya wengi wa macrush wale huwa ni ngumu kua ano
Kweli kabisa hujakosea Mwana!!! Daa!! Nilikuwa nako! bana kanaitwa Josephina Shana kabinti ka Daktari wa kijiji, Hukooo Tarime sehemu moja inaitwa Kibumaye, hakika Jose ulinikaa moyoni bwana wee! uko wapi Baby!!! nilikapenda hako ni hakuna tena kijiji kizima!!
Moyoni mwangu kalikuwa kazuri sana kwa hali na Mali hata iweje nilikapenda Mno nikafa kasoro kuoza, kiasi hata kangefanikiwa kunizaba vibao nisinge mudu kujibu zaidi ningekaangalia tu kujikuna !!! nakusamehe kwa dhati ya moyo!
Yaani nilikuwa nikikaona tu hivi wajameni Mwili unakufa ganzi kabisaa!!! sisemi kitu kwake nilioza nikafa hai!! hapo ni hkn dawa jamani Mapenzi yapo wala si dawa!! Mbaya zaidi Mama yake mzazi alinipenda Mnoooo!!! alikuwa ni Nurse pale kijijini walifanana!!
But by then kuongea sijui!! kutongoza sijui!! Kuanzishaa swaga sijui !! hata kangenipa nisingejua niifanyeje wajameni!!! ila kakinisemesha kidoogo tu! daaa!! bwanawee siku hiyo raha yake haisemeki njia nzima mtu akiniona anajua nina furaha!
siku hiyo nita cheka na kufurahi njia nzima ka bwege hapo mtu yeyote niombe msaada uone nakupa kabisaa!! na siku hiyo yaani kulala ni vizuri mno!! ajabu sasa drsni mie nilikuwa dororooo!!
Lkn Jose wajameni Mwee!! kalinipita mbali mnooo!! kalikuwa kana ongoza kimasomo, Mwandiko, hesabu, kuimba mwee!! kanashika number one!! hakika kaliheshimika shule nzima!! acha Darsani tu!
Ule mpango wa kujipanga kimashindano team mbili, mnakimbia team moja huku na nyingine huku kwa kushika kijiti basi kalikuwa kanakimbia hako kuliko wote kakaitwa Rocket , hapo ndo kabisaa nikazidi kuoza!!
ile tunaanza mishe mishe za kujipanga nilikuwa najitahidi kupenya niwe na jose team moja!! nilikuwa naona raha mno! japo sikusemaga! wala hakakujua kabisaa! Daa!! Mapenzi bana!! yanaanzia Mbali sana wajameni pyuu!!
Mpaka leo Jose nampenda mnooo yani!! ila sijui yuko wapi anae jua jamani anisaidie!! sababu tu mie ni mkweli nitajua uongo na ukweli!! nikimpata haijalishi ameolewa au haja olewa mimi na yeye!! yeye na mimi walipo hama kijijni sijawahi onana nae tena!!
kwa mara ya mwisho nilisikia yuko Bwasi kijijini ni Mwalimu!! awe hai awe mfu namtaka Jose! Mapenzi yangu kwake hayakuishia palepale tu yako hai mpaka leo na kesho pia !!
Lkn maajabu sasa kabinti hata mpango na Mimi hakakuwa nao Kabisaa!! drsani nilikuwa Mjinga pyuu!! hata kusoma sikujua!! ila kuandika ndo ulikuwa hunitoi!! Nilishangaa kusikia kaka yake alikuwa Polisi Mkubwa tu kafariki juzi juzi tu hapa!!