Unamkumbuka Deborah Mwenda wa Radio Tanzania?

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,277
Reaction score
8,860
Nimekutana Mlimani tv na mahojiano ya mtangaziji wa zamani sana Radio tanzania "RTD" anaitwa Debora mwenda dah huyu mama sasa ni mzee na sasa hivi anamiliki shule ya msingi bahari beach
Ki ukweli nilivutika sana enzi hizo na vipindi vyake hususani vile vya "Chei chei" na "Mama na mwana
Anasema amestaafu mwaka wa 1995 ana watoto 4 kwa sasa
Yapi mnayokumbuka enzi ya vipindi vya bibi huyu?sio mbaya tukikumbushana hapa ilikuwaje na ulikuwa wapi enzi hizo?Tv alikuwa anaangalia mwalimu nyerere tu.
 
aahhh nimemkumbuka saana..enzi hizo saa nane flani mchana umeshashibaaa mnazunguka redio kuanza kusikiliza hadithi ya kibibi jitu..aisee alivokuwa anasimulia na vionjo vyake basi unaona kama kweli na woga unakujia ukitengeneza mazingira ya kutisha kichwani mwako...daahhh shida yake usiku hata kwenda chooni unataka usindikizwe..aisee zamani maisha yalikuwa na ladha sana..siku hizi..ukimueleza mtoto kuna rtd kwanza anakushangaa..keshazoea tamthilia za runingani...mara mafb...instagram..puuuhhh ndo maana ubunifu umepotea miongoni mwa watoto
 
Daah umenikumbusha mbali sana unakumbuka hadithi ya akajase mbamba na ua jekundu, binti chura, n.k
 
Daah umenikumbusha mbali sana unakumbuka hadithi ya akajase mbamba na ua jekundu, binti chura, n.k

Nakumbuka Ablessed ilikuwa shida
Kuna mtu kasema digi alikuwa akikutuma dukani inapotimu saa 8 mchana unanuna balaa kanigusa maana nilikuwa mlevi sana wa kipindi cha mama na mwana
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…