Betri zinaanikwa juani ili ziwe na nguvu zisikorome.Halafu zinafungwa kwenye rula za mianzi zina kuwa nyiiiiingii
Jumamosi baada ya Deborah Mwenda, kinafuata kipindi nadhani JUNGU KUU km sikosei! Baada ya hapo tunajiunga na matangazo ya mpira ya moja kwa moja!
Nakumbuka hadithi ya binti chura ilinisisimua sana,mmoja wa wahusika aliitwa Imani kama sijakosea.Dah,long time maeneo ya Songea enzi hizo.Ule utoto ulikuwa mzuri sana
Naona kashinda Tuzo leo... hongera zake
Tuzo gani vile?
Saa nane jumamosi duh halafu redio ya mkulima
Halafu unakumbuka mchezo wa redio wa kina mzee jongo , hiyo ilikua usiku saa mbili kama sikoseiKuna ule wimbo nyalileee nyalilee babu zimwi nipe motooo mnaitikia nyalilee nkawipikie wanangu mnaitikia tena nyalilee
Kweli mkuu tena hata shule kama za day kwa hapa dar tulikua tunakunywa chai ya maziwa + mkate na chakula kizuri kumbuka hiyo sio bweni. Imebaki hadithi hata watoto wetu tunapowaambia mambo hayakua hivi hawaaminiGood old times,wengi tulifurahia maisha,serikali ilikuwa serikali yenye kujali watu wake,watu ni wazalendo wenye upendo wa kweli,wabunge wengi walikuwa ni waalimu walioshawishiwa na wananchi kuwa viongozi (Si maprofesa au wahindi na waarabu kama sasa).Mambo mengi yalikuwa ni mazuri kwa kweli
Halafu unakumbuka mchezo wa redio wa kina mzee jongo , hiyo ilikua usiku saa mbili kama sikosei
Na Aloisia ManenoMtangazaji mwenzie na huyu Deborah Mwenda aitwae Sarah Dumba katangulia mbele ya haki.
Mchezo ulikuwa mzuri sana ule. Mle ndani yuko Mzee Jongo, Mama Haambiliki, Matuga...aisee siku zimepitaHalafu unakumbuka mchezo wa redio wa kina mzee jongo , hiyo ilikua usiku saa mbili kama sikosei