Unamkumbuka Deborah Mwenda wa Radio Tanzania?

Unamkumbuka Deborah Mwenda wa Radio Tanzania?

Jumamosi baada ya Deborah Mwenda, kinafuata kipindi nadhani JUNGU KUU km sikosei! Baada ya hapo tunajiunga na matangazo ya mpira ya moja kwa moja!

Baada ya Debora Mwenda kilifuatia kipindi cha kina Umulkheir nadhani kama sio Deutche Welle ni Sauti ya Umoja wa mataifa....
 
Nakumbuka hadithi ya binti chura ilinisisimua sana,mmoja wa wahusika aliitwa Imani kama sijakosea.Dah,long time maeneo ya Songea enzi hizo.Ule utoto ulikuwa mzuri sana
 
Good old times,wengi tulifurahia maisha,serikali ilikuwa serikali yenye kujali watu wake,watu ni wazalendo wenye upendo wa kweli,wabunge wengi walikuwa ni waalimu walioshawishiwa na wananchi kuwa viongozi (Si maprofesa au wahindi na waarabu kama sasa).Mambo mengi yalikuwa ni mazuri kwa kweli
 
Nakumbuka hadithi ya binti chura ilinisisimua sana,mmoja wa wahusika aliitwa Imani kama sijakosea.Dah,long time maeneo ya Songea enzi hizo.Ule utoto ulikuwa mzuri sana

Mkuu unakumbuka hadithi ya shuweya? Unasikiliza mpaka damu zinakimbia, unadhani lile jitu litatokeza kwenye redio.
 
Du mmenikumbusha mbali wakuu,Mimi hadithi ya Kibibi Jitu had I nilikuwa silali
 
Sijawahi kusikia kipindi chake chochote
 
Ua jekundu, adili na nduguze, binti chura hlf anatia na vionjo kama unaangalia movie acha kabisa
 
Kuna ule wimbo nyalileee nyalilee babu zimwi nipe motooo mnaitikia nyalilee nkawipikie wanangu mnaitikia tena nyalilee
Halafu unakumbuka mchezo wa redio wa kina mzee jongo , hiyo ilikua usiku saa mbili kama sikosei
 
Good old times,wengi tulifurahia maisha,serikali ilikuwa serikali yenye kujali watu wake,watu ni wazalendo wenye upendo wa kweli,wabunge wengi walikuwa ni waalimu walioshawishiwa na wananchi kuwa viongozi (Si maprofesa au wahindi na waarabu kama sasa).Mambo mengi yalikuwa ni mazuri kwa kweli
Kweli mkuu tena hata shule kama za day kwa hapa dar tulikua tunakunywa chai ya maziwa + mkate na chakula kizuri kumbuka hiyo sio bweni. Imebaki hadithi hata watoto wetu tunapowaambia mambo hayakua hivi hawaamini
 
Mtangazaji mwenzie na huyu Deborah Mwenda aitwae Sarah Dumba katangulia mbele ya haki.
 
Sauti yake ilikuwa very soothing, hadithi ndo usipime!
sijui yuko wapi!
"Mama na mwana"
 
Halafu unakumbuka mchezo wa redio wa kina mzee jongo , hiyo ilikua usiku saa mbili kama sikosei
Mchezo ulikuwa mzuri sana ule. Mle ndani yuko Mzee Jongo, Mama Haambiliki, Matuga...aisee siku zimepita
 
Back
Top Bottom