Unamkumbuka Deborah Mwenda wa Radio Tanzania?

Unamkumbuka Deborah Mwenda wa Radio Tanzania?

Akajesembamba..xhura...mi nilijua ni za kweli hehehe
Halafu sasa chura akiwa anaongea,anammuliza mme wake kwa nini huna raha,kijana anajibu mfalme kasema kila mke wa mwanae atendeneze zuria jekundu,ule utoto ulikuwa poa sana
 
Nakumbuka Ablessed ilikuwa shida
Kuna mtu kasema digi alikuwa akikutuma dukani inapotimu saa 8 mchana unanuna balaa kanigusa maana nilikuwa mlevi sana wa kipindi cha mama na mwana
Saa nane jumamosi duh halafu redio ya mkulima
 
Nimekutana Mlimani tv na mahojiano ya mtangaziji wa zamani sana Radio tanzania "RTD" anaitwa Debora mwenda dah huyu mama sasa ni mzee na sasa hivi anamiliki shule ya msingi bahari beach
Ki ukweli nilivutika sana enzi hizo na vipindi vyake hususani vile vya "Chei chei" na "Mama na mwana
Anasema amestaafu mwaka wa 1995 ana watoto 4 kwa sasa
Yapi mnayokumbuka enzi ya vipindi vya bibi huyu?sio mbaya tukikumbushana hapa ilikuwaje na ulikuwa wapi enzi hizo?Tv alikuwa anaangalia mwalimu nyerere tu.

Aisee hizi zilikua enzi nzetu tuko Mapambano P School Sinza darasani nikuadithiana tu na kuimbiana "babuuu zimwiii niipee motooo, nyali nyalileeee, nikapikie wanaaanguu nyali nyalileee cha waliii na cha mchuuziii nyali nyalileee
 
Ua jekundu, adili na nduguze, zamani kiwango cha furaha kilikuwa juu sana. Sasa hivi watu wanafuraha za artificial tu.

Hapo zamani kulikuwa na amani mtaani, vijana walivuta bange tu, hapakuwepo na cocain
 
Umenikumbusha mbali sana hadithi ya mtoto wa mfalme kumwoa chura unaikumbuka hiyo? Ilikuwa bonge la simulizi.
 
Halafu sasa chura akiwa anaongea,anammuliza mme wake kwa nini huna raha,kijana anajibu mfalme kasema kila mke wa mwanae atendeneze zuria jekundu,ule utoto ulikuwa poa sana

Huyo Chura ndio binti mrembo Vaselisa.
 
Huu uzi una ubaguzi flani hv, ngoja tuwaachie wakongwe mtiririke.
 
dah umenikumbusha mbaaali, miaka hiyoo nilipokuwa home..hadi mazingira ya home nayakumbuka, ilikuwa tunaizunguka redio ya mzee kipindi cha mama na mwana, hadi watu wakubwa walikuwa wanasikiliza kipindi ambacho kilikuwa cha watoto..ilikuwa sipitwi yani kila siku ya jumamosi mchana lazima nichapwe kwa kuchelewa madrasa..yaani nilishajitolea kuchapwa na ustaz kila jumamosi kuliko kukosa mama na mwana..

watoto wa siku hizi hawana vitu vizuri jamani
 
Huu uzi una ubaguzi flani hv, ngoja tuwaachie wakongwe mtiririke.

ha ha hauna ubaguzi ....na wala si zamani sana...kipindi hicho when RTD was RTD ....utake usitake utaisikiliza tu haikwepeki.....
 
Duh! miaka hiyo free stress! kwanza ile beat yake tu ilikuwa burdani sogea kidogo miaka ile umkute mzee jangala la kundi lake la mandela wakidhaminiwan na chibuku mchezo wa radio duh waqt umeenda wapi?
 
Huu uzi una ubaguzi flani hv, ngoja tuwaachie wakongwe mtiririke.
Si hivyo kijana wakti umekuweka pembeni tu hata sie tunapata tabu sana na ktuni zenu za ben10!
 
Zamani raha ukitaka kusikiliza nyimbo za bendi zetu unaanza na kombora hapo unapata burdani au ombi lako hapo sasa nafsi inatulia ah waqt umekwenda wapi? siku hizi radio nyingi lakini ladha hupati ila kwa vijana wa leo hamuwezi kuiona tofauti coz hamkuwepo.
Acha tujimwage mwage wala hauna ubaguzi mleta uzi chukua gwala kwa kuuleta.
 
Komboraaaaaaa 05:30 Alfajiri hiyo acha tu
 
Alijua kuitumia sauti yake barabara, poa alikuwa na sauti yenye ushawishi kwa watoto na watu wazima, wengi tuliamini kama si hadithi bali ni hali harisi.
Hatukuwa na television lakini tuliburudika kuliko watoto wa kipindi hiki cha .com.
 
Jumamosi baada ya Deborah Mwenda, kinafuata kipindi nadhani JUNGU KUU km sikosei! Baada ya hapo tunajiunga na matangazo ya mpira ya moja kwa moja!
 
Back
Top Bottom