Na Mwandishi Wetu, Arusha
Ni vigumu kuamini kuwa aliyekuwa Denti wa Yunivasite ya Mtakatifu Augustino pale Nyegezi Mwanza ambaye bado anatafunwa na skandali ya upigaji wa picha za ngono, Nsia Swai amezua jambo jipya lenye lebo ya kituko cha aina yake, Ijumaa halina cha kuacha kuripoti.
Kizazaa cha Nsia Swai kimekuja kufuatia kuonekana kwa sura yake katika meza ya majaji wa shindano la ulimbwende mkoani hapa akivalia cheo cha jaji wa mamisi wanaoandaliwa kwa ajili ya kumpata Miss Tanzania 2010.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na macho ya Ijumaa lilijiri katika Ukumbi wa Hoteli ya Naura Springs mjini hapa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo kulikuwa na kinyanganyiro cha kumsaka Vodacom Miss Arusha City Center 2010 huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Raymond Mushi.
Katika ishu hiyo iliyohudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi kutoka Kenya, Mhe. Samweli Poghisio, jambo lililozua utata ni utambulisho wa Nsia Swai kama mmoja wa majaji wa shindano hilo.
Soon baada ya introdakisheni hiyo, baadhi ya wahudhuriaji walisikika wakinongona kuwa, mtu mwenye kashfa ya kupiga picha za utupu iweje awe jaji wa mamisi huku wakitaka nafasi hiyo ichukuliwe na watu ambao ni watakatifu katika macho ya jamii.
Hiki ni kituko cha aina yake, huyu si ni Nsia Swai ambaye aliripotiwa katika vyombo vya habari kupiga picha chafu? Sasa iweje awe jaji wa mamisi? Hii nafasi ilipaswa kupewa mtu safi mbele ya jamii, alisema mmoja wa wafuatiliaji wa kinyanganyiro hicho ukumbini humo ambaye jina lake halikunaswa mara moja.
Aidha, wadau hao walikwenda mbele zaidi na kudai kwamba, kumekuwa na dhana potofu kuwa mashindano ya mamisi ni uhuni au umalaya hivyo ni lazima waandaji wawe makini ili kudhihirisha kuwa ni shindano lenye heshima fulani nchini.
Unajua baadhi ya wazazi wanaona mashindano haya ni uhuni au umalaya, sasa ili kuweka mambo sawa ni lazima hata majaji wake wawe ni watu fulani ambao hawana skendo, alisema mdau mmoja aliyetambulika kwa jina la Eliufoo.
..Nsia akiwa miongoni mwa majaji
Hata hivyo, baadhi ya wadau walionekana kuwa tofauti ambapo walidai kwamba, kuvuja kwa picha za Nsia halikuwa kati ya agenda zake kwani ilitokea kwa bahati mbaya kufuatia umafia aliofanyiwa hadi kusambaa kwa foto hizo.
Waliendelea kupasha kwamba, si vema kumhukumu mtu kwa jambo baya moja alilofanya bila kukusudia huku mazuri yenye hesabu za maelfu yakisahaulika.
Ilisemekana kwamba, Nsia bado anayo nafasi ya kuonesha kuwa ni mkali katika fani ya urembo kwani waliompa shavu la ujaji hawakumpa bure bali walizingatia vigezo husika na uzoefu alionao katika mambo ya urembo.
Mjadala ulichukua kasi mithili ya moto wa kifuu ambapo kama siyo msanii kutoka pande za Kenya, Jackson Ngechu CMB Prezoo kuitwa stejini na MC wa shughuli hiyo ambaye ni Presenta wa Kituo cha Runinga cha EATV, Dominic Nyalifa ili kutumbuiza na baadaye Zahra Seleman kujinyakulia taji hilo kwa mwaka huu, basi diskasheni ingeendelea hadi mwisho.
Nsia na mwenzake, wakiwa madenti wa chuo (wakati huo, kwa sasa wamehitimu) waliripotiwa kupiga picha za utupu zilizozagaa kila kona ya nchi zaidi ya mwaka mmoja uliopita ambapo ishu hiyo iliwafanya kupata misukosuko ya ajabu chuoni.
KWETU SISI
Nsia ni mrembo jasiri anayepaswa kutosikiliza maneno ya kumkatisha tamaa na badala yake kusonga mbele ili kudhihirisha kuwa yeye ni mwanamke mrembo, msomi na mwenye kuona mbali kwa ajili ya maisha ya baadaye.-MHARIRI.