Wakuu naomba kuweka kidogo hapa,
1. Ninaamini kuwa Babu alikuwa ni mmoja kati ya best African intellectuals, infact nikiwa College US tulitumia kitabu chake kimoja, kwenye darasa la international politics, kwa hiyoi kweye hili la usomi, alikua ni aliyebobea sana.
2. Now tatizo langu na Babu, ni uongozi wake kisiasa kwa sababu nina wasi wasi kuwa either hakuna enough history ya records zake, au hazikuwepo kabisa, au mwenye kujua vyema atuweke sawa hapa exactly where are his political leadership records? Alifanya nini kama kiongozi?
3. Yeye na Mwalimu walikuwa na political standing ya namna gani hasa? Kwa sababu Babu was very much involved na deal nyingi chafu za kisiasa underground, lakini Mwalimu always looked the otherway ni kwa nini hasa?
- Kwa sababu according to the CIA, Babu aliwahi kuwapeleka wanafunzi wa ukomandoo Cuba, kati ya hao wanafunzi kumi aliowapeleka huko walikuwemo Salim na Mahafudhi, na kwamba nia na madhumuni ya Babu ilikuwa ni one day waje waipindue the then serikali ya Karume, na ni moja ya sababu kubwa sana US waliyoitumia kumnyima Salim, ukatibu wa UN.
4. Mauaji ya Karume yalipotokea Babu alikuwa ni mmoja wa tuhumiwa kule visiwani, lakini akakimbilia bara ambako Mwalimu, alimmuweka lupango lakini kwa mazingara ya utatanishi sana na baadye alimuachia huru, sasa swali langu ni how Babu aliweza kuwa this lucky? Je alikwua na uadui na kisiasa na Mwalimu au kuna ukweli ambao hausemwi?
Kwa kumaliza ninaomba ksuema hivi, kwa kweli mimi ni mmoja wa wananchiw aliokuwa disappointed na Babu na Kambona, kwa sababu walipokuwa nje nilisikia sana sifa zao, nikaamini kuwa mawazo ya Mwalimu yanaenda un-challenged kwa sababu watu kama wao hawapo bongo, kwa hiyo siku wakirudi itakua patashika ya Chua ngoma na Juma Mrisho.
Lakini that was the case, siku walipoamua kuhutubia wananchi Jangwani nilikuwa mmoja wa wananchi wa kwanza pale kiwanjani, lakini hata kabla hawajamaliza hotuba zao, niliona kama wananchi wengine walivyoamua kuwa ni bora kujiunga na maandamano ya Mtikila, yaliyokua yanapita pale kutokea Magomeni kwenda Kariakoo kwa sababu yalikuwa yana-make more sense kuliko hawa wakulu.
Ndio nikajifunza one thing, kwamba Mwalimu pamoja na mapungufu yake mengi sana yasiyosemeka, alikua ana akili sana huenda kuliko wananchi wote waliokuwepo Tanzania wakati tunapata uhuru, au?