GT,
Babu hatasahaulika just for the fact that he was an intellectual who put his intellect to work. Alijitahidi kuandika vitabu na hivi vitasaidia kuweka historia yake. Unlike Kambona ambaye aliishi Uingereza God knows kwa miaka mingapi. Alishindwa kuandika hata kitabu kimoja tu kuelezea tofauti kati yake na Nyerere. By the way Babu was also a friend so I am a bit biased.
Mkuu Jasusi utakuwa hutendi haki kumfananisha Prof.Babu na Mzee Kambona.Wanafanana kwa sifa moja tu kwamba "wote ni waanzilishi wa Taifa letu Tukufu Tanzania",Lakini ni watu waliokuwa na mitazamo Tofauti....Wakati Babu alikuwa kada wa Mashariki,Mzee Kambona alikuwa anatazama zaidi Magharibi ya akina Kennedy kama ilivyokuwa Mwalimu Nyerere....Marehemu Nyerere alikuwa Rafiki wa Karibu wa Oscar Kambona kuliko Babu ambaye alionekana kama Mjamaa Mzanzibari.Nyerere alianza kuwa Mjamaa baada ya Ziara ya China na kuanzishwa kwa Azimio la Arusha - 1967.
Mara ya mwisho kukutana na Prof.Babu ilikuwa Harlem,New York Novemba'90 kwenye Warsha iliyoandaliwa na organization ya Malcom X (RIP) ambayo Prof. Babu alizungumza, Warsha iliyokwenda kwa Title: "Radical Tradition & a Legacy of Struggle".Mwalimu Babu alikuwa na mahusiano ya karibu na Malcom X,inaelezwa kuwa Malcom na Babu walikutana mara ya kwanza July'64 huko Cairo kwenye Uzinduzi wa O.A.U,Wakati huo Babu akifuatana na Mwalimu Nyerere,Prof. Babu akiwa Waziri ktk Jamhuri ya Muungano.Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume.
Prof.Babu alizaliwa Zanzibar na alipata Elimu yake UK ambako ndiko alikokimbilia baada ya kutoka Jela 1978/79.Katika maisha yake ya ujana Prof.alijifunza sana Ujamaa wa Mashariki,alikuwa kipenzi wa Afrika na Mwanamapinduzi wa kweli.....alishiriki katika kampeni na kumshauri Rais Nkrumah na hatimaye kushinda Urais wa Ghana 1956.
Kwa upenzi wake wa Siasa za China na Mfumo wa Ujamaa aliweza kukutana na Viongozi wakuu wa Mataifa ya kijamaa kama Mao Tse Tung,Waziri Mkuu Chou En Lai,Marshal Chen Yi na muasisi Deng Tsiao Ping.Pia aliwahi kuwa mwandishi wa kujitolea wa Chinese News Agency (HSINHUA).Ikumbukwe kuwa Ziara aliyoifanya Mwalimu Nyerere na Prof.Babu huko China ndiyo iliyomfanya Mwalimu aupende Ujamaa na kuanza kuvaa Chon en Lai (Suti za kichina),na kufuatia Ziara hiyo ndio ukaanza Mgongano wa kimtazamo kati ya Mwalimu na Mzee Kambona ambae alikuwa na mtazamo wa kimagharibi zaidi, mgongano huo ulimfanya Mzee Kambona ajiuzulu Uwaziri.
Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana,lakini ni wazi kuwa kwa tabia ya Nyerere si rahisi kukaa karibu (Zizi moja) na mtu anayemzidi akili au kuwa tishio ktk misimamo yake,na ndio maana urafiki wake na Kawawa na Munanka ulidumu kwa muda mrefu,kwa sababu waungwana hao hawakuwa challenge kwake...ni watu wa Yes Sir!! kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.Babu aliondoka Tanzania kwenda US mwaka 1978/79 baada ya kifungo...na baadaye aliondoka US kuhamia UK.
Kwa mnaotaka kuona maandiko mahiri ya Prof Babu someni kitabu kiitwacho "African Socialism" alichoandika akiwa Jela,Prof Babu atakumbukwa zaidi kwa juhudi zake binafsi kama Waziri, za mazungumzo na hatimaye Ujenzi wa Reli ya Tazara......kwa wale waliopo USA wanaweza kupata maelezo ya kuvutia yamuhusuyo Babu kwa kuzungumzana Prof Ali Mazrui (Boston) au kwenye Kumbukumbu za Malcom X,Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.
Kaka GT Shukran kwa kuleta kumbukumbu ya huyu Mwanamapinduzi!!