Unamkumbuka kwa yapi Abdul-Rahman BABU?

Unamkumbuka kwa yapi Abdul-Rahman BABU?

Kuna mtu anayeweza kunikumbusha ilikuwaje Babu na u-intellectual wake wote akakubali kuja kufanya siasa chini ya Mrema ndani ya NCCR-Mageuzi? Sikumbuki vyema lakini nadhani NCCR walijaribu kumfanya kuwa mgombea mwenza wa Mrema lakini ikashindikana!

Naomba nieleweke kwamba namuheshimu sana Babu na vitabu vyake navisoma sana hadi sasa. nataka tu kujua ilikuwaje akakubali kurudi kwenye siasa kupitia mlango huo!
 
Hilo lisikushangaze hata kidogo kwa sababu kuna watu mpaka leo wanaamini Yesu alitembea juu ya maji lakini hawaamini kama kuna kitu kinaitwa kusoma nyota

Halikadhalika inaonekana hukuwahi kwenye kwenye mikutano ya Mohammed Dedes pale kinonondoni Boafra, jamaa alikuwa anaongea lugha ya kiinterlectual kwenye ushaguzi ulijaa matusi na watu walikuwa hawamuelewi

Na more interestingly jiulize Lupumba na uprofessa wake wote ilikuwaje akawa anaburuzwa na Maalim Sefu na wale na mediocre wengine waliojazana pale CUF
 
ndgu zangu wanaJF;

Leo nimejifunza historia ya Tanganyika. imenifungua mimacho. Please vitu kama hivi nahisi ni muhimu hapa jamvini kupunguza hasira za matukio haya.

Asanteni wachangiaji wote kuanzia na mtoa hoja GT,
 
Abdul Rahman Babu ndiye injinia wa siasa zilizoshindwa za ujamaa na kujitegemea na zile za vijiji vya ujamaa Tanzania.

Nyerere alikuwa haujui ujamaa wa kikomunisti maana shule zote alizosoma Nyerere zilikuwa za kikatoliki na vyuo alivyosoma vyote ukomunisti haukuwemo kwenye mtaala wa masomo yake.

Kilichotokea ni kuwa alipata mori wa Tanganyika ipate uhuru ijitawale.Ila nadhani hakujua vizuri ikipata uhuru iende kwa siasa ipi? Ndiyo maana miaka ya mwanzo ya uhuru huoni Nyerere akitamka kuwa Tanzania itakuwa ni nchi ya yenye kufuata siasa ipi zaidi ya porojo.

Sasa baada ya Tanzania kuungana na Zanzibar alimchukua Mzanzibari Abdulhaman babu na kumpa uwaziri wa mipango ya uchumi ya nchi.Alipopewa ndipo akaanza kuandika kwenye gazeti la Nationalist la Tanzania kuhusu mawazo yake ya siasa za ujamaa na kujitegemea.

Hapo ndipo akaanza kumfundisha Nyerere kuhusu ukomunisti na ujamaa ambao kwa Nyerere lilikuwa somo jipya ambalo hajawahi kulisikia wala kulifanyia mazoezi na mtihani lakini linalovutia kusikiliza.Na kwa sababu Nyerere alikuwa msomi akamwamini sana msomi mwenzie Babu kwa vile alivyokuwa akisema vyaweza leta faida.Na ni kipindi hicho hicho ndipo na Nyerere naye alipojifanya kinara wa ujamaa kwa kuanza kuandika vitabu kama FREEDOM AND SOCIALISM akiandikia ujamaa anaouita wa Kiafrika (AFRICAN SOCIALISM) ambao haujawahi fanyiwa majaribio popote katika Afrika yeye akaanza kujifanya Nabii mwafrika mwanzilishi wa huo ujamaa koko! Na msemaji wake maarufu na akaamua Tanzania ndiyo iwe nchi ya kuanzia ya kujaribishia huo ujamaa ambao haujawahi kuwepo.

Nyerere akazidi kumwamini Babu akamwachia injinia huyo wa siasa ya ujamaa zilizoshindwa kabla ya kuanza ajaribu hayo mawazo yake ya kindoto kwenye mipango ya uchumi ya Tanzania kama waziri.

Siasa ya ujamaa ikaingizwa na kutangazwa kama sera ya nchi na siasa ya kufuatwa na nchi kipindi hicho cha Babu alipokuwa waziri.Marafiki zetu wakaanza kuwa wachina,warusi,wakorea na wa-cuba ambao ndio waliokuwa walimu wakuu na viranja kwenye shule na seminar alizoenda Babu ambao Babu alikuwa akinukuu mawazo yao kwa kila akisemacho na aandikacho.

Walichokosana na Nyerere ni kuwa baada ya kumwamini Babu na mawazo yake ya ujamaa slikuja kuona hayasaidii nchi kwenda mbele na hayatekeleki kuanzia vijiji vya ujamaa,maduka ya ushirika,Azimio la Arusha n.k kuonekana vinadorora

Nyerere alianza kumwona Babu kama tapeli wa kisiasa aliyemchuuza mchana kweupe na kuua umaarufu wake ili aonekane hafai mbele za wananchi kwa kumshauri vibaya kama waziri aliyemwamini.Akaona kila kilichozalishwa na Babu kwenye siasa za nchi hii kinakufa magotini kwake .Akaamua kumtema Babu na kuachana naye kwa hasira za kizanaki zilizochanganyika na za kikurya za kwa wajomba zake.

Akaachana naye kimya kimya na kumzira.Naye Babu akaondoka kwenda kufundisha na kuandika kuhusu huo ujamaa wake ambao haukuwa na mahali pa kuufanyia kazi zaidi ya madarasani na kwenye midahalo ya wasomi kwenye kuta za vyuo vikuu ya mashindano ya maneno yasiyo na vitendo vya kusaidia wananchi.Huko ndiko mtu maarufu lakini kwa mtanzania jamaa alitutia umaskini na sera zake huko wizara ya mipango alikokuwa.

Tunachojifunza ni kuwa Mtu anapotaka kuwa Raisi ni vizuri yeye mwenyewe ajue atafuata siasa au njia ipi.Kwangu mimi ni maraisi wawili tu ndio walijizatiti kuwa maraisi na walijua wanaenda kufanya nini ikulu ili kuifikisha nchi wanapotaka na wakaifikisha walipotaka.Maraisi wawili hawa ni wale wenye majina yanayoanzia “M” yaani Mwinyi na Mkapa .Mwinyi alipoingia aliingia na sera ya RUKSA kupata pesa kwa njia yoyote mtu uijuayo na kweli hiyo RUKSA ilifanya kazi maduka yaliyokuwa matupu yakajaa,Pesa za kigeni zikajaa,watu wakajaa mapesa n,k.Pamoja na mapungufu yake hadi leo anajulikana kama MZEE RUKSA watu wanajua alisimamia nini Ikulu na humshangilia kila apitapo kwa hilo.Na wengi husema hakuna kipndi watu walikuwa na hela kama cha Mzee Ruksa.

Mwingine ni Mkapa.Mkapa miaka mitano ya kwanza ya uongozi wake alisema anasimamia ukusanyaji mapato na ulipaji madeni ili nchi iweze kukopesheka.Miaka mitano iliyofuata akasema ni ya ujenzi wa miundo mbinu na akafanya hivyo.Pamoja na mapungufu yake yeye alimudu kufikia malengo yake na kila akipita kwenye watu hupiga makofi kuwa mwanaume agenda alizopanga zilifanikiwa.

Awamu hii ya nne ya JK wa pili (JAKAYA KIKWETE) bado sijajuwa kwa sentensi moja tu Raisi anasimamia nini? Naona porojo nyingi kama kipindi cha mwanzo cha Nyerere.

Naona naye kama vile alivyokuwa mwenzie JK wa kwanza (JULIUS KAMBARAGE) alitegemea Babu na huyu naye naona anategemea tu wanamtandao anaowaamini sijui ni kwa sababu ya uhodari wa kusema au upi walionao hofu yangu yasije kumkuta ya Nyerere na Babu wake kama hatakuwa na ajenda yake mwenyewe kama wenzie Mwinyi na Mkapa.
 
GT,
Babu hatasahaulika just for the fact that he was an intellectual who put his intellect to work. Alijitahidi kuandika vitabu na hivi vitasaidia kuweka historia yake. Unlike Kambona ambaye aliishi Uingereza God knows kwa miaka mingapi. Alishindwa kuandika hata kitabu kimoja tu kuelezea tofauti kati yake na Nyerere. By the way Babu was also a friend so I am a bit biased.

Mkuu Jasusi utakuwa hutendi haki kumfananisha Prof.Babu na Mzee Kambona.Wanafanana kwa sifa moja tu kwamba "wote ni waanzilishi wa Taifa letu Tukufu Tanzania",Lakini ni watu waliokuwa na mitazamo Tofauti....Wakati Babu alikuwa kada wa Mashariki,Mzee Kambona alikuwa anatazama zaidi Magharibi ya akina Kennedy kama ilivyokuwa Mwalimu Nyerere....Marehemu Nyerere alikuwa Rafiki wa Karibu wa Oscar Kambona kuliko Babu ambaye alionekana kama Mjamaa Mzanzibari.Nyerere alianza kuwa Mjamaa baada ya Ziara ya China na kuanzishwa kwa Azimio la Arusha - 1967.

Mara ya mwisho kukutana na Prof.Babu ilikuwa Harlem,New York Novemba'90 kwenye Warsha iliyoandaliwa na organization ya Malcom X (RIP) ambayo Prof. Babu alizungumza, Warsha iliyokwenda kwa Title: "Radical Tradition & a Legacy of Struggle".Mwalimu Babu alikuwa na mahusiano ya karibu na Malcom X,inaelezwa kuwa Malcom na Babu walikutana mara ya kwanza July'64 huko Cairo kwenye Uzinduzi wa O.A.U,Wakati huo Babu akifuatana na Mwalimu Nyerere,Prof. Babu akiwa Waziri ktk Jamhuri ya Muungano.Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume.

Prof.Babu alizaliwa Zanzibar na alipata Elimu yake UK ambako ndiko alikokimbilia baada ya kutoka Jela 1978/79.Katika maisha yake ya ujana Prof.alijifunza sana Ujamaa wa Mashariki,alikuwa kipenzi wa Afrika na Mwanamapinduzi wa kweli.....alishiriki katika kampeni na kumshauri Rais Nkrumah na hatimaye kushinda Urais wa Ghana 1956.

Kwa upenzi wake wa Siasa za China na Mfumo wa Ujamaa aliweza kukutana na Viongozi wakuu wa Mataifa ya kijamaa kama Mao Tse Tung,Waziri Mkuu Chou En Lai,Marshal Chen Yi na muasisi Deng Tsiao Ping.Pia aliwahi kuwa mwandishi wa kujitolea wa Chinese News Agency (HSINHUA).Ikumbukwe kuwa Ziara aliyoifanya Mwalimu Nyerere na Prof.Babu huko China ndiyo iliyomfanya Mwalimu aupende Ujamaa na kuanza kuvaa Chon en Lai (Suti za kichina),na kufuatia Ziara hiyo ndio ukaanza Mgongano wa kimtazamo kati ya Mwalimu na Mzee Kambona ambae alikuwa na mtazamo wa kimagharibi zaidi, mgongano huo ulimfanya Mzee Kambona ajiuzulu Uwaziri.

Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana,lakini ni wazi kuwa kwa tabia ya Nyerere si rahisi kukaa karibu (Zizi moja) na mtu anayemzidi akili au kuwa tishio ktk misimamo yake,na ndio maana urafiki wake na Kawawa na Munanka ulidumu kwa muda mrefu,kwa sababu waungwana hao hawakuwa challenge kwake...ni watu wa Yes Sir!! kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.Babu aliondoka Tanzania kwenda US mwaka 1978/79 baada ya kifungo...na baadaye aliondoka US kuhamia UK.

Kwa mnaotaka kuona maandiko mahiri ya Prof Babu someni kitabu kiitwacho "African Socialism" alichoandika akiwa Jela,Prof Babu atakumbukwa zaidi kwa juhudi zake binafsi kama Waziri, za mazungumzo na hatimaye Ujenzi wa Reli ya Tazara......kwa wale waliopo USA wanaweza kupata maelezo ya kuvutia yamuhusuyo Babu kwa kuzungumzana Prof Ali Mazrui (Boston) au kwenye Kumbukumbu za Malcom X,Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.

Kaka GT Shukran kwa kuleta kumbukumbu ya huyu Mwanamapinduzi!!
 
Babu na Mwalimu walikuwa na tofauti kubwa za kiitikadi, kidira na kimtizamo. Mwalimu aliuchukia na kuugopa Ukomunisti. Kuna wakati hata hakuruhusu vitabu vya Kikomunisti viingie nchini. Hilo ni jambo la kwanza tunalopaswa kukumbuka. Mwalimu hakuwa Mkomunisti. Alikuwa ni Msoshalisti wa Kiafrika, yaani Mjamaa na aliuiita Ujamaa kuwa ndio Msingi wa Usoshalisti wa Kiafrika. Na maandishi yake daima yanaupinga Ukomunisti na Umarxisti uliojikita katika dhana ya 'class struggle', yaani 'mapambano ya kitabaka'. Ndio maana alizima sana harakati za Vyama vya Wafanyakazi. Kwa Upande wake, Babu alikuwa Msoshalisti wa Kisayansi yaani Mmarxisti ila uzeeni alikuwa na mlengo wa kati.

Kabla hajafariki, Babu aliazimia kuandika kitabu cha kuelezea historia nzima ya maisha yake na jinsi yalivyohusiana na historia ya Tanzania/Zanzibar. Bahati mbaya aliishia kuandika muswada tu wa historia hiyo ambao ulichapishwa na E & D Limited mwaka 2001 ndani ya kitabu 'Babu: I saw the Future and it Works' kilichohaririwa na Prof. Haroub Othman. Zifuatazo ni baadhi ya dondoo kutoka katika muswada huo wa Babu zinazoonesha jinsi alivyotofautiana na Mwalimu:

...President Nyerere's declaration of 'socialism and self-reliance', arising out of his own frustration with the system he was presiding over, was unworkable precisely because of the defensive position the country was put in. This strategic weakness was compounded by the push for an alternative strategic outlook before any serious development plan could be launched. I discussed this point with many colleagues, most of whom were equally frustrated, but helpless to do anything about it. Every proposal I put forward, especially when I was made Minister of Trade, was frowned upon and obstructed by politicians as well as civil servants. Expatriates dominated the system of government, starting from State House, via the Treasury, down to all departments of government. What they did not approve of, they made sure would not be implemented. I'll discuss the alternative strategy I had in mind in some detail.

Nyerere's Arusha Declaration was taken seriously by the underpriviliged who saw it as a radical break with foreign domination. Although it had many theoretical and even practical weaknesses, most of us tried our best to make it work. It turned out, however, that our vision and Nyerere's vision on what the Declaration was about were divergent. He looked at it as a simple village effort for self-sufficiency, permanently reproducing itself on the same structure of production cycles, increasing the quantity of the cash crops which would bring in more money and gradually raise the standard of living of the villagers. In other words, his vision was improvement via quantity, not via qualitative change. I shared a different perspective, a perspective of improvement through structural change, of replacing the colonial economy with a national economy. Taken in the latter sense, the Declaration would have aimed at creating the material conditions for a rapid development of the productive forces, putting Tanzanians in charge of their own destiny....

Historians will probably locate the beginning of disintegration of the regime's leadership at the February 1972 unprecedented Cabinet reshuffle, which threw out some of the most experienced ministers, including myself, (altogether, a total of about one hundred years of combined cabinet experience - a serious manpower loss to the country). In our place, were appointed some very junior and inexperienced technocrats whose only qualification for such senior appointments was their total and uncritical loyalty to President Nyerere personally. They were all 'yes-men', described by Nyerere as the 'believers', as in religion (waumini in Kiswahili).

This new cabinet was the beginning of Tanzania's decline. Nyerere was getting impatient with the slow movement of people to the new Ujamaa villages...he immediately abandoned the previous principle of voluntary moves and embarked on a policy of forcefully evicting reluctant peasants from their old villages... In only a matter of months, the country experienced a serious shortage of food because the old villages no longer produced and the new ones were not yet ready to produce...The country was then forced to spend millions of borrowed dollars to import food. This was aggravated by the effects of the nationalisation of wholesale trade...The saga of trade nationalisation, which I had resisted as Minister of Trade, will be discussed at length, which I believe, contributed to the rapid decline of Tanzania's economy beginning in the early 1970s...

Hayo ni maneno ya Babu mwenyewe. Binti yake, kwa jina Salma Babu, pia amekusanya maandishi yake mengi tu na kuyachapisha katika kitabu cha 'The Africa We Need' alichokihariri pamoja na Amrit Wilson mwaka 2002 - mchapishaji wa kitabu hicho ni African World Press kutoka kule Asmarra, Eritrea. Nikipata muda nitadondoa mawazo ya Babu katika sura ya 'The Future that Works' iliyopo katika kitabu hicho na ambayo inaongelea mtizamo wake mpya wa mlengo wa kati usio wa kibepari wala wa kisoshalisti.

Afrika lazima iwe na miundo yake yenyewe badala ya kuiga tu ubepari wa Kimagharibi na usoshalisti wa Kimashariki!
 
..companero....naomba link nipate kusoma vitabu vya babu.....nimesoma mtazamo wake uliouweka hapo ./.umenipa kichaa kuona kuwa tanzania tulikuwa na watu makini kama hapa tukashindwa kuwatumia......

sijui ni lini pale chuo kikuu huwa wanapata muda wa kumjadili pof babu [kama mwanazuoni].............these heroes will soon be forgotten kama hakuna hata kitu kinachoitwa kwa majina yao...na kusoma maandiko yao,huo ni udhaifu wetu mkubwa..watanzania.
 
Mkuu bahati mbaya sina anwani za mitandao ya mada za Babu labda utafute kwenye gugo. Ila vitabu vyake ndio hivyo vipo na vinapatikana kwenye maduka ya vitabu hapa Tanzania. Chuo Kikuu wanamheshimu sana Babu na mwaka 2001 walikuwa na kongamano la kujadili hicho kitabu cha ' I saw the Future and it Works'. Maprofesa wanaomkubali sana Babu pale ni Chuo ni Issa Shivji na Haroub Othman na wote wameandika sura moja katika hicho kitabu. Sura ya Shivji inaitwa 'Babu: A Man of Continental Vision' na ya Othman inaitwa 'Comrade Abdulrahman Babu: A Revolutionary Internationalist'.

Inabidi na sisi tuwe na Mhadhara wa Kumbukumbu ya Babu kama walivyo nayo huko katika Chuo Kikuu cha London!
 
Abdulrahman Babu said:
Historians will probably locate the beginning of disintegration of the regime's leadership at the February 1972 unprecedented Cabinet reshuffle, which threw out some of the most experienced ministers, including myself, (altogether, a total of about one hundred years of combined cabinet experience - a serious manpower loss to the country). In our place, were appointed some very junior and inexperienced technocrats whose only qualification for such senior appointments was their total and uncritical loyalty to President Nyerere personally. They were all 'yes-men', described by Nyerere as the 'believers', as in religion (waumini in Kiswahili).

Campanero,

..reshuffle ya 1972 ilihusisha wafuatao: John Malecela[Foreign Affairs], Chediel Mgonja[elimu],Edward Sokoine[Ulinzi],Cleopa Msuya[Finance],....

..sijaweza kupata majina ya mawaziri wengine, haswa wale walioachwa kwenye mabadiliko hayo.

..pia sijui mawaziri "waumini/yes-men" wa sera za Mwalimu walikuwa ni wapi. the only name i could come up with ni Rashidi Kawawa.
 
Kuna mtu anayeweza kunikumbusha ilikuwaje Babu na u-intellectual wake wote akakubali kuja kufanya siasa chini ya Mrema ndani ya NCCR-Mageuzi? Sikumbuki vyema lakini nadhani NCCR walijaribu kumfanya kuwa mgombea mwenza wa Mrema lakini ikashindikana!

Nuru kama kuna historia ambayo imesahaulika kirahisi ni historia ya kuanzishwa kwa NCCR - Mageuzi. Watu wanadhani hiki kilianza kama chama kumbe sio. NCCR ulikuwa ni mkusanyiko wa watu wenye mwamko wa mageuzi, wakiwemo wanafunzi, wafanyakazi, wanazuoni n.k. Maana halisi ya NCCR ni 'National Convention for Constitutional Reform', yaani Kongamano la Mabadiliko ya Kikatiba. Huu ndio ulikuwa msingi wa NCCR hata kilipojiandikisha na kuwa chama cha kisiasa. Mwamko huu ulimvutia Mwanazuoni Babu kuungana na NCCR kabla Mamamluki hawajakivuruga kule Tanga walipozima taa gizani na kuanza kupigana kwa viti na stuli kwenye mkutano wa NCCR! Kwa maelezo zaidi soma mada hii: [media]http://www.jpanafrican.com/docs/vol1no9/AbdulRahmanMohamedBabu.pdf[/media] yenye dondoo hii:

Babu was approached by the NCCR Mageuzi to stand as a Vice Presidential candidate. The NCCR was an eclectic collection of groups including right-wingers, human rights lawyers and activists, disgruntled workers and peasants, radical youth and Machingas or street hawkers. Babu had long been committed to multi-party democracy; he felt he could not turndown the request. In August 1995 Babu returned to Tanzania to a massive and ecstatic welcome from the people. However he was eventually prevented from standing for election by the legal manipulations of the ruling party. As always putting political commitment before personal ego, Babu remained in the country tirelessly campaigning for the party. When the NCCR lost after massive rigging by the ruling party, Babu wrote two seminal pamphlets - 'Tanzania's first multi-party elections' and 'Wanted: a Third Force in Zanzibar Politics' - analyzing the situation and suggesting a way forward

Kisa chote cha jinsi kina Prince Bagenda walivyompa somo Babu mpaka akakubali kurudi Tanzania kujiunga nao kinajulikana na kimehifadhiwa katika maandishi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Nakala ya kisa hicho sinayo hapa. Nikiiona nitakupa dondoo.
 
kama natoka nje ya mada kumradhini.

wakati tukimzungumzia babu (rip) nadhani haitakuwa vibaya kuzungumzia pia wale ambao walikuwa na mtazamo unaofanana nae na jinsi walivyohusika kupenyeza mitazamo yao katika siasa za nchi yetu.

katika hili nitashukuru iwapo kuna mtu anafahamu zaidi michango ya mzee sheri taki (rip). nasikia mzee huyu alikuwa mmoja wa waumini wa siasa za kikomunist ndani ya sekretarieti ya tanu/ccm. ninachofahamu mzee huyu aifariki akiwa katika hali mbaya ya kiuchumi na mpweke.
 
Mkuu Jasusi utakuwa hutendi haki kumfananisha Prof.Babu na Mzee Kambona.Wanafanana kwa sifa moja tu kwamba "wote ni waanzilishi wa Taifa letu Tukufu Tanzania",Lakini ni watu waliokuwa na mitazamo Tofauti....Wakati Babu alikuwa kada wa Mashariki,Mzee Kambona alikuwa anatazama zaidi Magharibi ya akina Kennedy kama ilivyokuwa Mwalimu Nyerere....Marehemu Nyerere alikuwa Rafiki wa Karibu wa Oscar Kambona kuliko Babu ambaye alionekana kama Mjamaa Mzanzibari.Nyerere alianza kuwa Mjamaa baada ya Ziara ya China na kuanzishwa kwa Azimio la Arusha - 1967.

Mara ya mwisho kukutana na Prof.Babu ilikuwa Harlem,New York Novemba'90 kwenye Warsha iliyoandaliwa na organization ya Malcom X (RIP) ambayo Prof. Babu alizungumza, Warsha iliyokwenda kwa Title: "Radical Tradition & a Legacy of Struggle".Mwalimu Babu alikuwa na mahusiano ya karibu na Malcom X,inaelezwa kuwa Malcom na Babu walikutana mara ya kwanza July'64 huko Cairo kwenye Uzinduzi wa O.A.U,Wakati huo Babu akifuatana na Mwalimu Nyerere,Prof. Babu akiwa Waziri ktk Jamhuri ya Muungano.Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume.

Prof.Babu alizaliwa Zanzibar na alipata Elimu yake UK ambako ndiko alikokimbilia baada ya kutoka Jela 1978/79.Katika maisha yake ya ujana Prof.alijifunza sana Ujamaa wa Mashariki,alikuwa kipenzi wa Afrika na Mwanamapinduzi wa kweli.....alishiriki katika kampeni na kumshauri Rais Nkrumah na hatimaye kushinda Urais wa Ghana 1956.

Kwa upenzi wake wa Siasa za China na Mfumo wa Ujamaa aliweza kukutana na Viongozi wakuu wa Mataifa ya kijamaa kama Mao Tse Tung,Waziri Mkuu Chou En Lai,Marshal Chen Yi na muasisi Deng Tsiao Ping.Pia aliwahi kuwa mwandishi wa kujitolea wa Chinese News Agency (HSINHUA).Ikumbukwe kuwa Ziara aliyoifanya Mwalimu Nyerere na Prof.Babu huko China ndiyo iliyomfanya Mwalimu aupende Ujamaa na kuanza kuvaa Chon en Lai (Suti za kichina),na kufuatia Ziara hiyo ndio ukaanza Mgongano wa kimtazamo kati ya Mwalimu na Mzee Kambona ambae alikuwa na mtazamo wa kimagharibi zaidi, mgongano huo ulimfanya Mzee Kambona ajiuzulu Uwaziri.

Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana,lakini ni wazi kuwa kwa tabia ya Nyerere si rahisi kukaa karibu (Zizi moja) na mtu anayemzidi akili au kuwa tishio ktk misimamo yake,na ndio maana urafiki wake na Kawawa na Munanka ulidumu kwa muda mrefu,kwa sababu waungwana hao hawakuwa challenge kwake...ni watu wa Yes Sir!! kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.Babu aliondoka Tanzania kwenda US mwaka 1978/79 baada ya kifungo...na baadaye aliondoka US kuhamia UK.

Kwa mnaotaka kuona maandiko mahiri ya Prof Babu someni kitabu kiitwacho "African Socialism" alichoandika akiwa Jela,Prof Babu atakumbukwa zaidi kwa juhudi zake binafsi kama Waziri, za mazungumzo na hatimaye Ujenzi wa Reli ya Tazara......kwa wale waliopo USA wanaweza kupata maelezo ya kuvutia yamuhusuyo Babu kwa kuzungumzana Prof Ali Mazrui (Boston) au kwenye Kumbukumbu za Malcom X,Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.

Kaka GT Shukran kwa kuleta kumbukumbu ya huyu Mwanamapinduzi!!
Mwawado,
Haikuwa nia yangu kuwafananisha Babu na Kambona. Nilichotaka kufanya ni ku "contrast' hasa ukizingatia kwamba Babu aliendelea kumwaga cheche hata alipokuwa makimbizini Uingereza na Marekani wakati Kambona aliishia kwenye ulabu tu. That is the only point I wanted to raise about the 2.
 
Prof.Babu amekuwa Waziri ktk wizara mbalimbali na vipindi tofauti toka 1964 - 1972,Alipotuhumiwa kwa mauaji ya Sheikh Karume....Kimsingi Babu na Mwalimu Nyerere hawakukorofishana...kilichomkimbiza Prof.Babu ni ile shutuma ya Umma Party kuhusika na kifo cha karume.

Mwawado,

Kunyoosha rekodi ya yanayoandikwa katika majadiliano ya Historia za humu, Abdul Rahman Babu hakupoteza kazi yake kutokana na mauaji ya Sheikh Karume. Ila alifukuzwa ghafla kwenye baraza la Mawaziri, February, 1972, miezi miwili kabla ya mauaji ya Sheikh Karume, Aprili, 7, 1972. Sababu ya kufuzwa haiko wazi sana kwa wafuatiliaji wa siasa za Tanzania ya dola ya wakati ule, lakini chochote kilichokuwa sababu, uongozi wa Nchi ni lazima haukumtaka kwa sababu haukumsubiri hata arudi nyumbani, bali ulimtimua akiwa Addis Ababa akiwakilisha Tanzania katika mkutano wa Mawaziri wa Umoja wa Afrika. (1)

...Kwani hata jina la kiislamu la Malcom lilipendekezwa na rafikiye Babu,Jina hilo ni El-Hajj Malik El-Shabazz.

Si sahihi.

Na hapa pia, katika kuweka sawa rekodi za historia za humu, Malcom X hakupewa jina la El-Hajj Malik El-Shabazz na Abdul Rahman Babu. Jina hilo alikuwa nalo miaka kabla ya kukutana na Babu kwa mara ya kwanza Misri, Julai, 1964. Jina Shabazz na nadharia nzima nyuma ya neno hilo ililetwa kwake na kwa Weusi wenzie wa Marekani na aliyekuwa kiongozi wa kikundi cha "Taifa la Uislamu," Elijah Muhammad. Katika kitabu chake "Ujumbe kwa Mtu Mweusi wa Marekani" ndugu Elijah Muhammad kwa mara ya kwanza anatambulisha jina hilo na nadharia inayosema Weusi ni watu wa asili, wenye umahiri maalum waliotokea "Kabila la Shabazz," waliotengenezwa na mwanasayansi aliyekuwa na muelekeo tofauti na wenzake. (2) Hapo ndipo Malcom X alipolipatia jina la Shabazz. Malik ni "Mfalme," kwa Kiarabu, lugha ya dini yake ya Kiislam (Malcom ni jina lililokuwa linatumiwa na wafalme wa Scotland). Kwa hiyo, El-Hajj Malik El-Shabazz ni Mfalme (Malik au Malcolm) wa ukoo au kabila la Shabazz aliyepata kujihi Makkah. (3)

Na mwisho, kakukuwahi kuwa na Uzinduzi wa O.A.U, mwaka 1964, Cairo. Tukio hilo lilifanyika kabla ya hapo, kwingine, Addis Ababa, Ethiopia, Mei 25, 1963.

Ufunguo:

(1) Abdul Rahman Mohamed Babu: Politician, Scholar and Revolutionary
By Amrit Wilson, Visiting Research Fellow, University of Huddersfield, UK

(2) The Name Shabazz: Where Did It Come From? Islamic Studies vol. 32 no.1 (Spring 1993), page 73-76

(3) Encarta encyclopedia : Malcolm X - MSN Encarta
 
Abdul Rahman Babu ndiye injinia wa siasa zilizoshindwa za ujamaa na kujitegemea na zile za vijiji vya ujamaa Tanzania.

Nyerere alikuwa haujui ujamaa wa kikomunisti maana shule zote alizosoma Nyerere zilikuwa za kikatoliki na vyuo alivyosoma vyote ukomunisti haukuwemo kwenye mtaala wa masomo yake.

Kilichotokea ni kuwa alipata mori wa Tanganyika ipate uhuru ijitawale.Ila nadhani hakujua vizuri ikipata uhuru iende kwa siasa ipi? Ndiyo maana miaka ya mwanzo ya uhuru huoni Nyerere akitamka kuwa Tanzania itakuwa ni nchi ya yenye kufuata siasa ipi zaidi ya porojo.

Sasa baada ya Tanzania kuungana na Zanzibar alimchukua Mzanzibari Abdulhaman babu na kumpa uwaziri wa mipango ya uchumi ya nchi.Alipopewa ndipo akaanza kuandika kwenye gazeti la Nationalist la Tanzania kuhusu mawazo yake ya siasa za ujamaa na kujitegemea.

Hapo ndipo akaanza kumfundisha Nyerere kuhusu ukomunisti na ujamaa ambao kwa Nyerere lilikuwa somo jipya ambalo hajawahi kulisikia wala kulifanyia mazoezi na mtihani lakini linalovutia kusikiliza.Na kwa sababu Nyerere alikuwa msomi akamwamini sana msomi mwenzie Babu kwa vile alivyokuwa akisema vyaweza leta faida.Na ni kipindi hicho hicho ndipo na Nyerere naye alipojifanya kinara wa ujamaa kwa kuanza kuandika vitabu kama FREEDOM AND SOCIALISM akiandikia ujamaa anaouita wa Kiafrika (AFRICAN SOCIALISM) ambao haujawahi fanyiwa majaribio popote katika Afrika yeye akaanza kujifanya Nabii mwafrika mwanzilishi wa huo ujamaa koko! Na msemaji wake maarufu na akaamua Tanzania ndiyo iwe nchi ya kuanzia ya kujaribishia huo ujamaa ambao haujawahi kuwepo.

Nyerere akazidi kumwamini Babu akamwachia injinia huyo wa siasa ya ujamaa zilizoshindwa kabla ya kuanza ajaribu hayo mawazo yake ya kindoto kwenye mipango ya uchumi ya Tanzania kama waziri.

Siasa ya ujamaa ikaingizwa na kutangazwa kama sera ya nchi na siasa ya kufuatwa na nchi kipindi hicho cha Babu alipokuwa waziri.Marafiki zetu wakaanza kuwa wachina,warusi,wakorea na wa-cuba ambao ndio waliokuwa walimu wakuu na viranja kwenye shule na seminar alizoenda Babu ambao Babu alikuwa akinukuu mawazo yao kwa kila akisemacho na aandikacho.

Walichokosana na Nyerere ni kuwa baada ya kumwamini Babu na mawazo yake ya ujamaa slikuja kuona hayasaidii nchi kwenda mbele na hayatekeleki kuanzia vijiji vya ujamaa,maduka ya ushirika,Azimio la Arusha n.k kuonekana vinadorora

Nyerere alianza kumwona Babu kama tapeli wa kisiasa aliyemchuuza mchana kweupe na kuua umaarufu wake ili aonekane hafai mbele za wananchi kwa kumshauri vibaya kama waziri aliyemwamini.Akaona kila kilichozalishwa na Babu kwenye siasa za nchi hii kinakufa magotini kwake .Akaamua kumtema Babu na kuachana naye kwa hasira za kizanaki zilizochanganyika na za kikurya za kwa wajomba zake.

Akaachana naye kimya kimya na kumzira.Naye Babu akaondoka kwenda kufundisha na kuandika kuhusu huo ujamaa wake ambao haukuwa na mahali pa kuufanyia kazi zaidi ya madarasani na kwenye midahalo ya wasomi kwenye kuta za vyuo vikuu ya mashindano ya maneno yasiyo na vitendo vya kusaidia wananchi.Huko ndiko mtu maarufu lakini kwa mtanzania jamaa alitutia umaskini na sera zake huko wizara ya mipango alikokuwa.

Tunachojifunza ni kuwa Mtu anapotaka kuwa Raisi ni vizuri yeye mwenyewe ajue atafuata siasa au njia ipi...

Si kweli. Hoja yako haina ukweli japo hitimisho lako lina ukweli. Rejea maelezo yangu ya awali kuhusu tofauti ya kiitikadi kati ya Babu na Nyerere. Tusichanganye Ujamaa na Ukomunisti. Kamwe Ujamaa wa Mwalimu haukuwa Ukomunisti ndio maana mpaka kesho Wamarxisti wanampinga sana Mwalimu kwa kutofuata Usoshalisti wa Kisayansi. Tusiandikie mate wakati wino upo na wino ndio maelezo haya ya Babu mwenyewe kutoka kwenye huo Muswada wa Kitabu alichokuwa akiandike kuelezea nini hasa kilitokea kati yake na Mwalimu:

...Consequently,as the Foreign Minister of Zanzibar, I became a target of superpower intrigues of all kind...Having resisted both the CIA and KGB respective enticements, I was targeted for a political, if not physical, destruction. Both superpower secret agencies worked behind my back, with the support of some of my corrupt colleagues, in their effort to frustate the foreign policy objectives which the Revolutionary Government of Zanzibar stood for and which were designed to accomplish Zanzibar's development strategy. I'll elaborate the ingenious trilateral trade arrangement which was about to be entered into between Zanzibar, Indonesia (a major importor of our cloves) and Germany (GDR) which would have led to a Hong Kong-like industrial/commercial development, and how it was sabotaged by one of the superpowers.

I'll also discuss how, pushing Zanzibar into Tanzania, meant poverty for the people and almost permanent stagnation...I'll outline the vision we had of a prosperous future of Zanzibar, and its potential for creating an area of economic prosperity in the entire region. I will discuss the opportunities that were lost because of narrow political motivations and utter lack of vision.

Thes strategy of frustrating our economic strategy for development continued even after being moved to the Mainland as Minister of Planning, following the creation of Tanzania. Although the manouvre to create Tanzania was intended to undermine what was considered as 'communist encroachment' in the region, and to frustrate and weaken the radicals from Zanzibar, I refused to indulge in self-pity and instead, continued to put forward strategies which I believed would be of great benefit for Tanzania. Policy making in Tanzania, I found out to my utter amazement, was left entirely to the expatriates, and Tanzanians only obeyed what was laid to them. Although I was officially Minister of State for Planning, I was put in a position where I could neither plan nor fulfil any of my ministerial functions. It was a deliberate move...

Hayo ni maneno ya Babu yanayodhihirisha kuwa huo unaoitwa ukomunisti wake kamwe haukuwa na sehemu katika nadharia za Nyerere ambazo zilikuwa zinapinga Ukomunisti. Na hata kisa hiki hapa kutoka kwa mtu aliyekuwa 'shushushu' wa Mwalimu na mwenza wake katika kuupinga Ukomunisti, ajulikanaye kwa jina la Al Noor Kassum, kinaonesha ni jinsi gani Mwalimu aliwaweka pembezoni hawa wakomunisti ngangari kutoka Zanzibar ambao alilazimika kuwaweka katika baraza la mawaziri baada ya Muungano:

In the new [Union] government [of 1964] I was appointed Parliamentary Secretary, Ministry of Industries, Mineral Resources and Power...My Minister was Abdullah [Kassim] Hanga from Zanzibar. Before the change of portfolio, Mwalimu Nyerere called me in and told me I had a special role to play in the Ministry. 'You are needed there to help look after Hanga', he said.

It soon became clear that Mwalimu was right to be cautious. The Minister had to present his budget to Parliament and after writing his budget speech he sent it for me for my comments. On reading it, I found myself in a dilemma because it was full of radical ideas. So I went to Mwalimu and appraised him of the situation. 'I can change it to some extent but I think it will be very difficult. It really needs to be rewritten,' I told him. Mwalimu then suggested a solution: 'Why don't you tell Mr Hanga that since this is the first time he is presenting a budget, the President himself would like to have a look at his budget speech. Tell him I asked you to inform him of this.' So, Hanga and I went to the State House and sat with Mwalimu. After reading the speech, he told Hanga, 'This is an excellent speech but it needs a little bit of adjustment. Perhaps the Minister for Planning [the same AM Babu who is on record for complaining that he "was put in a position where" he "could neither plan nor fulfil any of" his "ministerial functions"] could sit down with your two Parliamentary Secretaries and go through the speech. They can fit it in with what we are doing on the mainland currently.' And of course, by the time we had finished with the text, it was an entirely new speech.'

Huyo ndio Mwalimu ambaye alidiriki kukubali hotuba ya Kikomunisti ibadilishwe ili iendane na nadharia zake za Kiliberali!Japokuwa huwa namfagilia sana Mwalimu narudia na nitarudia tena kuwa Mwalimu hakuwa Mkomunisti. Mwalimu alichanganya madesa ya Usasa wa Kimagharibi na Uasili wa Kiafrika kujenga nadharia ya Ujamaa kama msingi wa Usoshalisti wa Kiafrika. Na alichangia kwa kiasi kikubwa kujenga Taifa linalochanganya madesa ya Kimagharibi na kutegemea washauri wa Kigeni ndio maana mpaka kesho Wizara zetu za Mipango zimejaa Washauri Wataalamu wa Umaskini kutoka Ughaibuni. Mwalimu alikuwa Mmagharibi ndani ya ngozi ya Mwafrika.
 
Tusiandikie mate wakati wino upo na wino ndio maelezo haya ya Babu mwenyewe kutoka kwenye huo Muswada wa Kitabu alichokuwa akiandike kuelezea nini hasa kilitokea kati yake na Mwalimu:

Kwa kuwa hicho kitabu chenyewe cha Babu hakijachapishwa bado hayo ni mate na siyo wino.
 
tofauti ya communist/socialist idealogy kati ya babu na nyerere is exactly the same as what happened between che and castro. babu was a believer of chinese version of communism (as che was) and nyerere, the russian version.
 
Companero,

Mkuu ni ukweli usiopingika kuwa Abrahman babu ndiye mwalimu wa Nyerere ktk Ujamaa..
Maelezo ya babu yote yanatangulia Muungano wetu kwa maana kwamba dhumuni la Muungano halikuwa kabisa kuihusisha nchi yetu na Ujamaa kutokana na shinikizo la nchi za magharibi. hata huo uwaziri wa nchi za nje kwa Zanzibar ulidumu tu kwa muda (four month to be exact) wakati ASP wakiwatafutia dawa Umma party kuwaondoa kabisa kwa sababu chama hicho kilijulikana kama ni chama cha Kikomunist..Ukweli ni kwamba ndio waliopindua utawala wa Sultan, yatasemwa mengi kupotosha.. but that is the fact.
Pamoja na kwamba dhumuni la Muungano lilikuwa kulinda Mapinduzi yale lakini swala la Ukomunist ndilo lilikuwa kichwa cha habari.. na Nyerere alikuwa very interested na kichwa hiki - Abraham Babu..
Ndio maana baada ya Muungano ASP walifikiria wameshinda kuwaondoa Umma Party lakini Nyerere alijua kwamba anamhitaji Abraham Babu na vichwa vingine toka visiwani akawavuta bara kama serikali ya Muungano kwa maslahi ya bara..
Kwa hiyo mkuu kuna ukweli ktk maelezo ya Myahudi wetu Netanyahu..na sioni tofauti zenu isipokuwa historia yenyewe mnachanganya wakati.
 
pia kuna kitabu kingine cha babu kinaitwa African Socialism or Socialist Africa?
 
... na Nyerere alikuwa very interested na kichwa hiki - Abraham Babu..
... Nyerere alijua kwamba anamhitaji Abraham Babu na vichwa vingine toka visiwani akawavuta bara kama serikali ya Muungano kwa maslahi ya bara..

Sasa kwa nini alimfukuza kazi February, 1972 ?
 
Back
Top Bottom