Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Abel Loshilaa Motika, maarufu kama Mr. Ebbo, alizaliwa tarehe 26 Mei 1974 jijini Arusha na alikuwa msanii wa muziki wa hip hop kutoka Tanzania.
Alijipatia umaarufu wake kupitia wimbo wake "Mimi Mmasai" mwaka 2002. Nyimbo zake nyingine maarufu ni pamoja na "Bado" na "Kamongo" kupitia studio yake ya MOTIKA Records.
Mwaka 2003 aliteuliwa kuongoza kampeni ya serikali ya ubinafsishaji, ambapo alitoa nyimbo yake ya "Ubinaf-sishaji".
Alifariki dunia tarehe 1 Desemba 2011 kutokana na ugonjwa wa leukemia katika Hospitali ya Mission Usa River huko Arusha.
Je, unakumbuka Mr Ebbo kwa kipi?
Pia soma
- Ngoma gani unaikumbuka toka Kwa huyu mwamba Mr Ebbo?
- TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia