Unamlindaje Mwanao Mtandaoni?

Unamlindaje Mwanao Mtandaoni?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Namna ya Kulinda Usalama wa Watoto Mtandaoni

1. Zungumza na mtoto juu ya matumizi sahihi na salama ya mtandao

2. Mfundishe mtoto kuhusu taarifa binafsi na namna ya kuzilinda

3. Weka mipaka ya mambo ambayo mtoto anaweza na hawezi kuyafanya mtandaoni.

4. Muhamasishe mtoto kutoa taarifa endapo atakutana na tatizo mtandaoni

Ni muhimu kuwalinda watoto mitandaoni kwani wahalifu wa mtandaoni hujaribu kupata taarifa za siri kutoka kwao, hivyo elimu kuhusu hatari za kushiriki taarifa binafsi ni muhimu.

Pia Wanyanyasaji wa mtandaoni wanaweza kuwaathiri watoto kisaikolojia, hivyo watoto wanapaswa kufundishwa kuripoti vitendo hivyo ili kuepuka msongo wa mawazo

Aidha Mafataki wa mtandaoni (Online Sex Predators) huwarubuni watoto kuingia kwenye mahusiano yasiyofaa, na wazazi wanahitaji kufuatilia mazungumzo ya watoto ili kuhakikisha usalama wao
 
Namna nzuri ya kumlinda mtoto akiwa mdogo ni kumpa malezi yanayo faa.
Kumfundisha ajitenge na marafiki wabaya na yasio mema.
Kumlinda mtoto dhidi ya marafiki wabaya na kutambua mtoto wako ana marafiki wa aina gani.
Mfanye mtoto amujue Mungu awe mwenye imani na aipende dini.
Sikiliza matatizo ya mtoto wako na mtatulie shida zake kwa wakati.
Mtoto anapokua mkubwa siku zote atakua ameishi katika misingi ambayo mzazi alimjenga nayo wakati wa utotoni.
Kijana ama Binti, mzazi unapaswa kuzungumza nae kwa kila jambo tena kwa uwazi, hiyo itamfanya mtoto wako asikuogope na awe huru kuuliza ama kusema changamoto yeyote ambayo atakabiliana nayo.
Zungumza na watoto kuhusu afya na mahusiano pia itawafanya wajitunze na waweze kujiamini na wachague wenza sahihi pindi wanapo anza kuingia kwenye magusiano.
 
Back
Top Bottom