GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Wakati wengine wanasema bora kwenda kazini kuliko kushinda na watoto na mzunguko wa kazi za nyumbani, kuna mtu hayo ndiyo maisha yake.
Atafanya kazi za nyumbani kama kupika, kufua, kuosha vyombo, kusafisha nyumba na wakati mwingine kuangalia mifugo ya nyumbani kama kuku.
Lakini bado ana jukumu la kuhudumia watoto. Wanaamka pamoja saa 11 alfajiri kuwaandaa waende shule na analala wa mwisho kwani majukumu yake ni mengi. Kwa kifupi msaidizi wa ndani ni wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala.
Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya wasaidizi wa nyumbani (house keepers day), swali ni je, huwa unampa nafasi msaidizi wako wa ndani wa kwenda kutembea, kubadilishana mawazo na wengine?
Ikiwa unafanya hivyo ni kila baada ya muda gani? Kwa kuzingatia umuhimu na ubinadamu wao, watu hawa wanahitaji angalau siku ya kwenda kupumzisha akili.
Chanzo: mwananchi_official
Na nimuonavyo tu wangu huko aendako pale nikimpa Mapumziko yake, hakika huwa anashughuliwa Kunakotukuka.