Unamsaidiaje Mtu ambae Akili zake Zimehama/Zimeruka?

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,600
Reaction score
59,760
Wakuu, msaada wenu naomba msaada kwenye jambo.

Hivi unamsaidiaje mtu ambae akili zake zimeruka?. Yaani mwanzoni alikua na akili timamu kabisa ila ghafla tu anageuka kua FYATU anaanza kuongea vitu vya ulimwengu ambao hauonekani kwa macho, unamsaidiaje?

Halafu nyie mnaozushia watu wanaumwa/wanaugua UKIMWI hali ya kuwa wenyewe wanaogopa kwenda kupima wanaanza kuwehuka na kuweweseka acheni hizo tabia, UKIMWI haupimwi kwa Macho.

Unamsaidiaje mtu ambae akili zimeruka?
 
Mpeleke hospitali kubwa kunakuwa na wataalamu wa magonjwa ya akili wao ni rahisi kujua changamoto ilipoanzia na suluhisho lake pia pamoja na dawa zitakazomsaidia ikiwa italazimika kutatua tatizo.
 
Kwa sasa ni kawaida hii dunia watu wanapata Depression sana. Na matibabu yanapatikana hospital anarudi kuwa sawa. Nimeshashughulika na watu aina hiyo kwa kuwapeleka hospital.

Hujataja jinsia lakini
 
Usisahau kumkumbusha kula chakula..
 
Hiyo imetokana na stress ya muda mrefu ambayo imesababishwa na sababu hizo hpao chini ikafikia kupata anxiety, depression na panic attacks. Mpeleke hospital kubwa yote kama Muhimbili au Milembe kitengo cha afya ya akili watampa dawa kumstabilize kwanza ili aweze kulala muda mrefu kutuliza neurochemical imblances ambazo ambazo zimepelekea hiyo bipolar disorder.
Ni muhimu kwa daktari pia ajue chanzo kilichopelekea hiyo situation aidha kwa kumuuliza mwenyewe kama anajiweza au kwa waliomzunguka ambao wataelezea kilichopelekea hili tatizo kwa kumuangalia (observe) wakiwa naye muda mrefu
 
Halafu nyie mnaozushia watu wanaumwa/wanaugua UKIMWI hali ya kuwa wenyewe wanaogopa kwenda kupima wanaanza kuwehuka na kuweweseka acheni hizo tabia, UKIMWI haupimwi kwa Macho.
Hii nayo usiipuuzie. ukichelewa kupata dawa ubongo unapata fungus mwishowe ndo huko kuchanganyikiwa. ukiwahi anapona japo ni ngumu sana kupona mtu akishafika apo.
 
Hiyo ni bipolar one ... Asipotumia dawa vizur itampata bipolar two....
Atumie haloperidol na sodium valparin , haloperidol na cabamazipine, haloperidol na lamotrigine
 
Hospital au metaphysical things.
 
Arudishwe tu kizimkazi kuna namna tena
 
Kwanza apimwe ukimwi kama anao au hana ksha mambo mengne yaendelee, khs kuongea mambo ya ulimwengu mwngne ni kweli upo ulimwengu watu wanaishi kabisa maisha yanaendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…