Unamshauri nini Aunt Ezekiel kuhusu ugomvi na Wema?

Unamshauri nini Aunt Ezekiel kuhusu ugomvi na Wema?

Abatmwe

Senior Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
110
Reaction score
79
Kwa kuangalia historia ya Wema Sepetu na Aunt Ezekiel ni zaidi ya marafiki ambao walikuwa maswahiba walioshibana kiasi kwamba hakuna mtu anaeweza kujua kama leo watakuwa maadui. Na urafiki huu ulikomaa zaidi pale Madame Wema alipokuwa amerudiana na Diamond Platinumz kiasi kwamba hata safari za nje za Wema na Diamond na Aunt nae alikuwa anasafiri na hatukujua alikuwa anasafiri kwa gharama ya nani.

Kwa ukaribu huu wa Wema na Diamond kulimfanya Dogo wetu Moses Iyobo kupata bahati ya mtende kilaini kwa dada yetu Aunt Ezekiel ambaye walianza mapenzi chini chini na kuficha kila walipoulizwa kama wana uhusiano ila alikataa, ila mwisho ya yote yalikuja julikana baada ya Aunt Ezekiel kupata ujauzito.

Sasa ikawa hawana jinsi lazima waweke wazi. Hatujui kama Madame Wema au Diamond alitumika kupiga pande kwa hawa wapenzi wawili ama la ila chanzo ni yeye kuwa na ukaribu na Diamond na Aunt Ezekiel ndo kukampa mwanya Moses Iyobo nae kuwa na uhusiano na Aunt Ezekiel.

Sasa leo kuna kamtihani kamemkuta Aunt Ezekiel kwa kuwa Madame Wema ameachana na Diamond Platinumz, na kuachana kwao kumetengeneza mgongano mpaka kupelekea kuwa na Team Diamond& Zari na Team Wema. Kwa kuangalia kwa umakini zaidi Aunt Ezekiel anakaribia kupata mtoto na Moses Iyobo na Upande mwingine bado yuko na Uswahiba na Wema Sepetu.

Aunt Ezekiel anapata mtihani kwa kulazimishwa na Wema kuwa bado awe kwenye Team Wema wakati yeye tayari ana usiano na Moses Iyobo ambaye ni Dancer wa Diamond na ukiangalia kwa umakini kila itakavyokuwa lazima Moses ndo anauhusika na kila kitu kwa huduma za Aunt Ezekiel.

Sasa ukiangalia kwa mbali kuna ugomvi wa chini chini kati ya Wema na Aunt Ezekiel ikisemekana kama Wema hataki Aunt Ezekiel amsapoti Diamond ila naamini Aunt Ezekiel anafanya ivi kwa mapenzi ya mpenzi wake Moses Iyobo.

Ukiwa kama wewe mdau unaweza mshauri nini Aunt Ezekiel;

1- Aaache kumsaport Diamond kwa kulinda urafiki wake na Wema?

2- Aache kumsaport Wema ali ajenge uhusiano zaidi na Moses Iyobo na kwa faida ya mtoto wao?

3- Au afanya uamuzi gani kwa hawa wahasimu wawili ili aweke mambo sawa kwa pande zote mbili.

Tumshauri dada yetu please bila matusi
 
Aunt aaangalie maisha yake na mpenzi wake mapenz ni ya wawili bana na afanye kile kitakachompa faraja na furaha
 
mbona kule IG wamepost picha ya pamoja nakuwachamba mlioshangilia ugomvi waoo
 
huwa napenda sana kutoa ushauri lakini kwa mambo kama haya huwa naangalia ushauri wa wengine.
 
Hapasio pahala pa kuzungumzia mamboya Wema na Aunty Ezekiel
 
Anti abaki kwenye msimamo wake. Yeye mwenyewe kasema haya:-

"Mimi sidhani kama hapo kuna ugomvi, maana nilichoandika na kuweka siku hiyo ilikuwa ni utani lakini hata kama yeye na ndugu zake walichukulia ‘siriasi' basi bado walitakiwa kutambua kuwa, mchumba wangu Iyobo (Moses) ni mfanyakazi halali wa kundi la muziki la Diamond (Nasibu Abdul), hivyo nilikuwa na haki ya kumsapoti kwa asilimia zote maana fedha anazopata kupitia huko ndizo zinazonifanya mimi na familia yangu niishi," alisema Aunt.

Kama familia yake wamefikia hatua ya kuingilia hili, mimi nafikiri sina tatizo maana nina maisha yangu na yeye (Wema) ana maisha yake. Ila tu kama ni ishu ya wazazi, naomba wajue pia mimi sijajizaa wala sijazaliwa na miti, nina ndugu tena wanajitambua kwa kila hali.
"Nikiangalia sababu za ugomvi ni za kibinafsi sana hata hazifai kuingiliwa na mtu, maana haiwezekani kwenye maisha haya eti Wema akinuniana na mtu basi na mimi nimnunie, sijaumbwa hivyo wala sina unafiki huo.

"Kama staili ya maisha ikiwa kila atakayekwazana naye na mimi nimchukie siku wanapoelewana mimi si nitaonekana sifai kote? Wao wafahamu kuwa mimi najitambua wala si wa kuburuzwa hivyo.Kama wanasema hawawezi kushiriki lolote kwangu hata mimi sina sababu ya kujipendekeza kwao
 
Hata ili pia limeondolewa, kuna uongo apo?
 
Asiwe mnafiki kila mmoja ana wahisani wake,na sio vyema kama Wema amegombana na Diamond na yeye ndio asionge wala kusalimiana na watu,kwani yeye Aunty asio ongea nao yeye na Wema pia haongei nao....?????????????
 
Kama aliweza Petit-Man kuwa na dada wa Diamond huku akiwa na uhusiano mzuri tu na Wema kwanini ashindwe Aunt?
Issue ni trust na kutopelekwa au kujiingiza katika migogoro isiyo na kichwa wala miguu kwa lengo la kuunufaisha upande mmoja
 
ujinga mwingine
ugomvi wa wengine uingilie unamhisu
mtu wenyewe kigeu geu kesho wakirudiana na dai
anty mnataka aweke wapi sura yake...
 
Back
Top Bottom