Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kwa hekima na busara akae tu kimya na kujifunza kufuatilia kwa umakini maoni na mitazamo ya wengine, huenda akajifunza na kuongeza ufahamu na uelewa wa masula hayo muhimu yanayoweza kumsaidia huko mbeleni?
Ama apumzike au kuendelea na shughuli zake nyingine, huenda akatumia muda wake vizuri kwa faida?
Au akurupuke hivyo hivyo bila kua na maoni au mtazamo chanya bali tu bila sababu ya msingi aamshe mihemko, ghadhabu, kutukana na kuporomosha matusi mazito mazito ambayo hayana maana, hayasaidii wala kubadilisha chochote bila sababu ya msingi?
Unamshauri nini mtu kama huyo aliefikia ukomo wa fikra mbadala na mawazo au maoni mapya dhidi ya mada mbalimbali zinazowasilishwa na wangwana humu jukwani,
Maana saa zingine makasiriko ni mengi bila sababu japo inasikitisha na kutia huruma sana...
nadhani inafaa na muhimu sana kutokukata tamaa katika kujenga utamaduni wa kukubaliana kutofautiana kistaarabu bila matusi...
Nadhani hili ni muhimu zaidi kwa mustakabali mwema wa umoja, utangamano, amani na utulivu miongoni mwetu, kama familia muhimu na pana sana ya JF Tanzania 🐒