Mkuu, una majina mawili nini? Naona umechanganya mambo. Nashindwa kukuandika kwenye listi kwa sababu umeweka jina tofauti na jina lako la JF
Mkuu Luteni,
Wana siasa siku zote huwa wanasema Ahhh, sitaki, ahh hadi nimuulize mke wangu. Ni nchi chache sana ambazo kuna hiyo tabia ya kuanza kampeni mapema na kusema wazi kabisa ntagombea. Hata Kikwete sasa alikuwa akisema hivyohivyo. Kasema nini Dr. Slaa hilo si muhimu. Kwanza tunataka kuona anajiamini bila kujali kama atakosa kura au vipi. Kwani Karatu alianza vipi hadi akashinda? Tena huko alianza akiwa hata hafahamiki. Sasa hivi Dr. Slaa ni jina kubwa na ningelitegemea sasa awe msemaji kutoka CHADEMA kwenye hili swala la Wafanyakazi. Ni kipindi cha kutumia Lugha mbaya ya viongozi wa CCM na kujifagilia.
CCM hawajawahi kupata upinzani mkubwa kiasi hiki. Sasa wamekuwa kama Simba aliyejeruhiwa na wako tayari kumrarua mtu yeyote. Ila ukikutana na Maboxer wazuri kama Mohammed Ali au Johnson, ndiyo kwanza watazidi kukutukana kuwa ".... he wee vipi, mama yako anapiga zaidi kuliko wewe...." Sasa wewe zidi kuchukia na rusha makonde ovyo na uchoke. Hapo anakutwanga kama mtoto mdogo. Atakayekuwa Mvumilivu wa Kupokea mapigo ndiye atashinda.
Mwisho hii listi ni kutaka tu kumuonyesha kuwa tuko wengi wenye imani naye. Tanzania ni nchi ya Demokrasia. Na ni hilo leo hii tunalilaani na hivyo hatuwezi kumshambulia wala kumlazimisha mara akikataa. Kumbuka maneno ya jana ya Kikwete ya Mbayuwai kuwa "Akili za kuambiwa na changanya na akili zako......" Huyu nii Dr. wa sheria na nina imani muono wake utakuwa hata juu zaidi yetu sisi. Angelikuwa na imani na misimamo ya Watanzania ninaamini angeligombea na akamshinda Kikwete. Ila sisi ni Kigeugeu sana.
Clinton aliwaambia Wanyarwanda kuwa "mkikaa kujadiliana, hakuna uhakika mtaafikiana ila msipokaa basi hakuna kuafikiana". Na sisi tunapojaribu kuweka listi, hakuna uhakika kama Dr. Slaa atakubali ila TUSIPOJARIBU basi tuna uhakika kabisa kuwa HATAGOMBEA.