Elections 2010 Unamuunga mkono Dr. Slaa kugombea URAIS mwaka 2010? Jiandikishe hapa

Binafsi ningependa kuona Dr.Slaa akigombea,kwa kweli tuna ombwe la uongozi

hata hivyo,mwenywewe amesema hatagombea Urais,ingawa akibadilisha msimamo ,i will move heaven and earth to support him
 
Well Sikonge bado naamini Dr. atatusaidia kwenye mambo mengine tofauti na urais, ni hazina kubwa kwa vijana tusii expose sana ikayeyuka, ukiona adui yako anakushangilia jua kuna walakini some where, hebu fikiria kwa nini sisiem wanasema hawaoni mwingine zaidi ya Slaa? ukifikiria kwa makini mantiki yao is divide and rule they want to import to people's mind that Chadema is nothing but Slaa.
 

Asiyekubali kushindwa si mshindani. Kashafumua SIRI kibao na ma SKENDO kibao Tanzania. Kuna kilichobadilika? Inabidi sasa Dr. Slaa aende hatua moja mbele. Mwanzo wa ngoma ni lele. Unatudharau kuwa tuko 4% siyo? Yale yale ya kusema Wafanyakazi wako laki tatu na nusu. Ila tuna ndugu, jamaa na marafiki na tukianza kampeni za nyumbani, zinaweza kuwa na nguvu zaidi ya unavyodhani.

Ahh, hiyo ya acheni kichaa, una bahati leo siku nzuri maana ningelikuambia neno la Kikuli wa bandarini.
 
Bila shaka natakiwa kuwa juu ya list....
Sio tu nataka Dr.Slaa agombee Urais the the sake of it...
Hii ni nafasi MOJA tu ya mgombea tofauti na nafasi za Wabunge ambazo zipo zaidi ya 200. Umuhimu wa mtu huyu mmoja unachukua nafasi kubwa ya ushindi wa Wabunge 150 ambao ndio pekee wanaweza kuleta mabadiliko bungeni..Kukosekana kwa mtu mmoja ktk ushindi hakuwezi kuleta mabadiliko bungeni haswa ukizingatia kwamba CCM will make sure wanashinda zaidi ya nusu.. Uchaguzi Zanzibar ni alama tosha kuwakumbusha madudu ya C CM.
Ushindani kwa JK ni muhimu sana ukizingatia tawala za nchi za Kiafrika - Winner takes all ina maana zaidi ya ushindi wa majimbo.
 
I agree with you but not at red, ulivyosema kwenye red ni sawa na JK alivyosema hata wafanyakazi laki tatu wakimnyima kura atashinda tu hajui impact ya hao laki tatu kuwa wanawakilisha wapigakura wangapi.
 

Mkuu Mkandara tupo kwenye NJIA MOJA na ombi lako limetekelezwa kwa kukuweka wa Kwanza. Ila tu nimeweka namba 1. kwa mwenyewe Dr. Slaa na wewe nimeshakuweka namba mbili na hii haitabadilika.
 
please DR Slaa gombea tafadhali









 
Kama Dr. Slaa agombee urais wa JF mimi naona anafaa sana...nchi si lelemama nyie...Obama keshaota mvi tele kwa stress.
 
Dr.Slaa wana-usirudie makosa ya Mbowe... Ikiwezekana hamna haja ya CHADEMA kumsimamisha mgombea URAHISI... Kila mtu ajikite jimboni mwake...
Cha muhimu ni kuharibu kura za Mkwere... Ndio MKWERE...yeye si ametuita Mbayu-wayu Loh!!!
 
Nkwingwa...nami natofautiana nawe...Dr.Slaa akigombea kitakachotkea ni changamoto tu...piga ua mshindi atakuwa wa CCM,na akishindwa atakuwepo tu...upinzani bungeni utakuwa umelala doro....Ni vema akajipanga akagombea mwaka 2015 na mgombea wa CCM ambaye atakuwa ni mpya kwa kipindi hicho...yeye agombee tu ubunge mwaka huu ili ashinde na kuzidi kuleta changamoto na uhai wa opposition bungeni....Naomba agombee tu ubunge wa Karatu...Mbilinge mbilinge zake za bungeni bado zahitajika sana...pale anakuwa na uhuru sana wa kuongea na kuibua yasiyoibulika...Ningependa sana kumuona akiingia ulingoni 2015...Ni ushauri tu
 
Alpha

Just get rid of CCM. Enough is Enough, the country cannot afford five more years of these corrupt, incompetent fools.
 
21. Muhindi
 
Kama Dr. Slaa agombee urais wa JF mimi naona anafaa sana...nchi si lelemama nyie...Obama keshaota mvi tele kwa stress.
Junius unataka kuharibu uzuri wa thread urais wa bongo si sawa na wa US kule wanapima uwezo wa mtu kufikiri na kupambanua mambo urais wa Tanzania hata Kikwete anaweza bora liende.
 
Wakuu zangu,
Nitarudia maneno niliyoyasema mwaka 2005 baada ya Uchaguzi.
Kulingana na mazingira ya nchi za Kiafrika Kiti cha Urais ni muhimu sana kuliko position yeyote ile na itachukua ushindi wa Rais kuweza kubadilisha katiba, mfumo wa Utawala na hata kupunguza nguvu za rais.. Ni rais anayeweka sahihi mabadiliko ya aina yeyote kisheria..Muswada hauwezi kuwa act pasipo rais kuanguka..Akikataa kuweka sahihi kazi inarudi palepale kama haya maandamano. mtalalamika weee, hakuna kitakachobadilika. Hizi kelele za Bungeni tumeziona toka enzi ya NCCR -Mageuzi na hakuna policy yoyote iliyobadilika kwa sababu ya mawazo ya mbunge mmoja. Hata kama Dr.Slaa hatakuwepo bungeni watakuja kina Dr.Slaa wengine kuwakilisha mawazo ya Dr.Slaa. haikatazwi kwa Dr kusukuma hoja bungeni kupitia mbunge wake iwe Zitto au Mbowe..
Tumechoka na umaarufu, sasa hivi ni wakati wa kuishambulia CCM toka kona zote. Wahenga husema siri ya vita vyovyote ni kwanza muue Jenerali, utakuwa umeshinda vita. Ni maumbile ya viumbe wote duniani kumwondoa mtawala iwe nyuki, Simba au sisimizi. Hata Mapinduzi watu hulenga kwanza Ikulu na sii Bungeni.
Hivyo ifahamike kwamba tunachozungumzia hapa ni Mapinduzi ya Utawala uliopo.. Sii swala la kumwondoa JK madarakani. Huyu ni mtumishi tu wa chama ambaye tumeona kiburi akiwa mwajiri mkuu wa serikali, Mhimili tuliomkabidhi sisi wananchi kuungoza leo amekuwa kiongozi dhidi ya waliomwajiri..
Statement ya JK kuhusiana na wafanyakazi inatisha hasa anaposema hahitaji kura za Wafanyakazi... Haya ni maneno mazito sana ktk nchi yenye kutumia demokrasia na inabidi JK aombe msamaha! zipo lugha za kutumia lakini sii hii hata kidogo..
Nakumbuka hata Dr. Slaa mwenyewe kasema inabidi arudie kuisoma taarifa hiyo kwani haamini maneno hayo yamesemwa na kiongozi wa nchi aliyechaguliwa kwa kura. Na hii ni moja ya silaha kubwa ya mgombea dhidi ya JK kuwakumbusha wananchi hasa Wafanyakazi.

JK uongozi wa nchi umemshinda, hilo halina ubishi.. hata kina Yakhe sie tulokuwa na matumaini na mtoto wa Saigon tumebakia kushika matama yetu hatuamini kilichomtoa Kanga huyu manyoya. Hakika mgomo wa wafanyakazi ktk nchi maskini kama yetu inatisha sana lakini yeye kama Presidaa alitakiwa kulishughulikia hili miaka mitatu iliyopita badala yake zimeongezwa gharama ambazo hazikuwa na msingi wowote..Baraza la Mawaziri, Ndege na magari Mapya Ikulu, Chai na ongezeko la posho kwa mawaziri na viongozi wa serikali. Sasa hivi hata Madiwani na Halmashauri zinapewa fungu kubwa toka bungeni.. Hizi zote ni fedha za wananchi ambao wanalalamika kukatwa kodi kubwa ili kuendesha serikali hii..Sasa maswala kama haya tumsubiri Dr.Slaa hadi arudi bungeni jamani!
Ifike wakati nasi tuwe na mtu wa kuzungumza nje ya bunge..
 
Kama Dr. Slaa agombee urais wa JF mimi naona anafaa sana...nchi si lelemama nyie...Obama keshaota mvi tele kwa stress.

Junius,
Sikufahamu kwa hiyo sintakuhukumu. Ila jambo moja ambalo nina uhakika kabisa ni kuwa Dr. Slaa ni mtu pekee aliyepo hapa JF kwa sasa kama MBUNGE na anatumia jina lake halisi. Huo ni ujasiri tosha na hasa ukichukulia kuna watu wengine wenye maneno kama wamepata juice ya tende kama yako hapo juu. Siyo lazima uchangie kila kitu. Nilivyoona unajadili swala la Muungano nikafikiri una upeo mkubwa sana ila ghafla yakaanza ya Karume alikuwa hajui kusoma, hajui Kiingereza (Mmalawi na baharia huyoo hajui Kiingereza) na maswala mengine, nimeanza kukufahamu kwa ukaribu. Endelea kujifunua. Ila jambo moja tu ni kuwa kama Wanaotaka UHURU wa Zanzibar watu wenyewe ndiyo kama nyie, basi kweli naweza kukubaliana na Nyerere kuwa "nyie watu jamjakomaa kujitawala". Hebu onyesheni kukua basi kidogo hata kwenye majadiliano ya kawaida kabisa.

Wakati watu wanajadili mambo mengine, wewe unakuja na mambo ya RAIS wa JF, nakuona sawa kabisa na huyu Mzee hapa chini:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…