SoC02 Unan'tega?

SoC02 Unan'tega?

Stories of Change - 2022 Competition

Nabii koko

Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
21
Reaction score
15
Nikitazama sura yako, mwenendo wako, matendo na mavazi yako, nashindwa kuelewa, hivi unanitega? Huo mwendo sasa ndio kabisa unanichanganya. Ama umejua kwamba nami nategeka? Hiyo mikao yako ya ajabu ajabu umegundua kuwa unaniua ndio maana huachi kunichokoza? Ahaaa, kumbe umegundua hapo ndipo ulipo udhaifu wangu ndiyo sababu unanifanyia hivi?

Sasa sikiliza.... Mimi mwenyewe mjanja Kama wewe. Unayoyafanya wewe leo, wenzako waliyafanya enzi hizo. Hiyo mitego yako nimeishitukia na nakwambia hivi, sidanganyiki!

Ninalisema hili kwa sababu hata huyu mwenzangu ulishawahi kumtega kama mimi na akaingia kingi, kwa hiyo sisi ni wahanga wa mitego yako ewe MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA) pamoja na SHIRIKA LA VIWANGO NCHINI (TBS).

Haya yaliyonikuta kwa sababu yako ndiyo yaliyanifanya hii leo nifumbue mdomo.

SIO SIRI TENA! Siku hiyo nilikwenda kwenye duka linalouza vyakula mbalimbali vya kusindikwa. Ilikuwa ni baada ya mke wangu kushindwa kutoa maziwa ya kutosheleza kumnyonyesha mtoto wangu wa miezi sita. Nikaamua kuingia dukani kununua maziwa ya laktojen ili kuongeza nguvu katika kunyonyesha. Kiukweli sikuwa nimechunguza tarehe ya mwisho wa matumizi ya bidhaa hiyo.

Niliendelea na matumizi karibia miezi miwili. Katika kipindi chote hicho mwanangu haukuwahi kipumzika kujinyonganyonga kwa maumivu ya tumbo na kujisaidia kwa shida. Baadaye Kuna daktari aliniuliza kuhusu aina ya chakula ninachompa, nilipomwambia akanishauri kuchunguza kama maziwa hayo hayajapita muda wa matumizi. Kweli kilikuwa kimeisha muda wake miezi karibia miezi sita. Nilipoacha tu, ndiyo ilikuwa ponapona ya mtoto.

Kabla ya hapo nilikwishawahi kuchanganyiwa chupa za juisi ya embe miongoni mwa chupa 20 za soda na juisi nilizojumua kwa matumizi ya nyumbani. Kwa bahati nzuri niligundua Hilo mapema na nilipomfuata muuzaji akasema hata yeye aliuziwa hivyo, Sasa angepeleka wapi?

Nilibaki njiapanda kwa kuwa hata sikujua kwa kutoa mashitaka yangu. Kilichoniuma zaidi ni huyu mtoto aliyekunywa maziwa, Yuko salama? Asijekuwa ndo kapapta magonjwa ya saratani itakuwaje?

Nadhani wapo wengi walio kama mimi ambao wamewahi kwenda dukani wakauziwa bidhaa zilizoisha muda wake wa matumizi na wakatumia bila kujua. Yaweza isiwe juisi, ila ni chakula ama kinywaji chochote kile Mfano: unga wa sembe, juisi, mafuta ya kula, soda, viungo vya chakula, blue band na vyakula vidogo vidogo (bites).

Mbali na hivyo, ni mara ngapi tunanunua Dawa za kilimo (viwatilifu), mifugo ama Dawa za kuulia wadudu nyumbani zikiwa zimepitwa na wakati? Kinapotokea kibaya ndipo tunapobaini kuwa tulinunua bidhaa isiyofaa. Nakumbuka Kuna rafiki yangu alibabuka na kutokwa vipele vingi katika ngozi baada ya kipuliza Dawa ya kuzuia nyanya zisidhurike na wadudu shambani.

Tukirudi kwa akina dada, wapo waliokwishakutana na kesi hizi katika matumizi ya vipodozi. Unakuta mara baada ya kutumia kipodozi fulani, anaanza kuota mapele juu ya ngozi, vidonda na hata Kansa ya ngozi. Urembo unageuka majuto.

Kuna wauzaji wa Dawa za binadamu pia wanaojali maslahi Yao bila kuzingatia afya ya mtumiaji. Mfano niliingia duka moja la jamaa yangu wa karibu nikakuta anabandua lebo hailisi za Dawa na kubandika mpya zilizogongwa mhuri wa kuchongwa.

Nenda mipaka inayounganisha nchi na nchi Kama vile Boda ya Tunduma, Kuna mafuta ya kula ya nchi jirani yanaingizwa nchini kwa njia za panya na kuwekewa lebo za Tanzania ili kukwepa mkono wa TRA. Kwa bahati mbaya watumiaji huzichangamkia kwa sababu ya Bei zake kuwa chini. Je Kuna usalama kiafya hapo? Haya, Kuna wafanyabiashara wanapenyeza vipodozi kwa staili hiyo hiyo, pombe na vyakula vya kusindikwa kwa ajili ya watoto maarufu Kama "Waka Waka" Je, tunazungumziaje usalama wake kiafya?

Wapo waliouziwa matairi ya pikipiki baiskeli au gari yakiwa hayana ubora licha ya kuwa na chapa ya TBS. Pia kuna bidhaa chungu mzima zinaingizwa nchini zikiwa hazina nembo ya TBS na zipo sokoni. Ndipo hapo tunashangaa ajali nyingi za barabara kumbe ubovu unaanzia kwa TBS ambaye hakuthibiti ubora wa tairi kabla ya kumfikia mtumiaji.

Mara nyingi tumesikia TFDA ama TBS wameteketeza Tani kadhaa za bidhaa zisizo na ubora ama zilizoisha muda wa matumizi. Haya mambo yanatokeaje ikiwa Kuna ukaguzi wa kutosha mipakani? Hebu tujiulize, ni bidhaa ngapi zinabainika kutofaa kwa matumizi ya binadamu na tayari zimeshatumika? Ni madhara kiasi gani tumeshapata pasipo kujua huu uozo?

Na vipi kuhusu uthibiti ubora wa bidhaa za wajasiriamali wa ndani? Wengi wanatengeneza bidhaa na kuziuza pasipo kuguswa na tbs, mfano karanga, majani ya chai, mafuta ya kupikia, siagi, maziwa, mafuta ya ngozi na nywele nk. Ukichunguza hizi bidhaa utagundua hazina hata kibandiko kinachoonesha mtengenezaji, Muda wa kutengenezwa Wala wa kuisha matumizi.

Hapa ndipo ninapojikuta kuwaza kuwa nahisi wewe mhusika wa kusimamia ubora na VIWANGO vya bidhaa UNANITEGA. HII Ni kwa sababu najua unajua uwepo wa uozo huu nchini na bado hakuna hutua stahiki hazichukuliwi. Ndiyo maana bado unaniletea bidhaa tamu, nyingi zenye kuvutia macho halafu unanitaka nijiahadhali. Unakumbuka like tangazo la "unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako?" Na bado linaisifia? Unakumbuka lile linalosema " Uvutaji wa sigara Ni hatari kwa afya yako?" Na bado linatangaza ubora wa sigara? SASA MBONA UNANIWEKA NJIAPANDA, AU NDIO UNANITEGA?

MAONI YANGU:
1.Kwa kiasi fulani nazipongeza mamlaka husika pale wanapovamia maduka, bohari za dawa na stoo kukagua bidhaa zilizopo. Lakini ni bora ukaguzi huu ukafanyika kabla ya bidhaa kufika dukani.
2. Mamlaka husika hazitoshi kupita kila mahali kukagua, hivyo Ni jukumu la kila mmoja kutoa ushirikiano kwa kuwafichua wanaouza bidhaa zisizokidhi VIWANGO.
3. Kila mnunuzi ana wajibu wa kuhakikisha anakagua tarehe ya utengenezaji na kuisha kwa matumizi ya kila bidhaa anayonunua.
4. Watengenezaji bidhaa wasiangalie faida binafsi tu, waangalie na afya za walaji pia. Mtumiaji akifa, Je kesho utamuuzia nani?

Tukizingatia haya yote, tutaepuka magonjwa yasiyo ya lazima hususan Kansa. ASANTE!
Screenshot_20220827-140647.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom