Unanua Gari Unakosa Parking unaamua Kulilaza Sheli

Unanua Gari Unakosa Parking unaamua Kulilaza Sheli

Rudi Darasani
Gari la mtu ambaye haukumchangia kununua linakuhusu nini, mbona wapo wanaolaza nje ya nyumba zao hakuna ukuta wala mlinzi, Weka Post zenye tija hata kama ya kila tunda kimasihara bora kwani huingilii maisha ya mtu.
 
Ni kwa nini usijenge kanyumba kako, uweke na kafensi ka kishikaji kabla ya kununua gari?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Unaweza jenga kajumba kako kazuri, ukaweka kafensi ka kishkaji kwa ajili ya kulaza gari halafu ghafla kuna mshenzi mmoja akafanya ujenzi kwenye njia inayokufikisha kwako. Inakua hakuna jinsi!!!
 
Mwalimu inasemekana watu maskini hujifanya kushauri waliofanikiwa (matajiri) ili nao waonekane wapo eti wanajua!

Mwalimu na magari wapi na wapi?
hahaha.. hakika hii post yako mpwayungu akiiona atakupa kongore
 
Mwalimu na gari! Usishangae! Mshahara ni mdogo Ila ukicheza na mikopo kwa kutumia akili yenye nidhamu ya pesa, utajenga nyumba na kagari ka ushikaji.
 
Kagari na shell kipi kina gharama kubwa??? Jibu ni shell, bilashaka precautions wanazochukua watu wa shell ili isiungue shell yao kwa makosa ya kibinadam ni kubwa sana maana ni hundreds ya ist ndio upate gharama ya shell moja

Sijamotiveti watu walaze gari zao shell
 
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.

Umetafuta vipesa vyako kwa kudunduliza hatimaye ukanunua ki Spacio chako au Ki - Ist halafu mwisho wa siku unaamua kwenda kukilaza Sheli!.

Hakuna mtu mwenye wivu na kagari kako lakini nakutahadharisha ya kwamba Sheli si sehemu salama!.

Ni vema ukatafuta Maegesho mahali pengine ambapo ni salama lakini si Sheli kwasababu tunafahamu wote lile ni eneo maalumu kwa ajili ya vimiminika vinavyolipuka.

Kama wewe ni mwenzangu na mie ambaye hako ka gari kako kakiungua unabaki kubung'aa bung'aa tena ni vema ukajihadhari mapema;

Lakini kama wewe ni sawa na kina Bakhresa sina ushauri na wewe kwasababu hata ka-gari kako kakiungua utanunua kengine.

Ni hayo tu.
Vipi hako kagari kakiwa chanzo cha ku unguza kituo cha mafuta!? Mana kina fundi maiko wanaweka sana mataa taa ya kichina mpaka kwenye matairi ya huto tu gari!
 
Unafunga ndoa huna nyumba unaamua kuishi na mkeo ktk nyumba za kupanga za wanaume wenzenu...
KATAA NDOA UISHI KWA AMANI UIMARIKE KIUCHUMI
 
TOKA NIZALIWE EARLY 90’s Ndani ya jiji la dar sijawahi sikia sheli iliyoungua na kuunguza magari.

Nikakumbuka Mwaka 2016 nilikua dalali wa magari, pale opposite na be foward zinapaki gari nyingi IT, with no risk.
Hizo sheli zinazounguza vigari ziko maeneo gani?

Nikajua utaandika risk ya kuibiwa
 
Umepatwa na nini mkuu! Maana si kwa povu la uzi wako! Mtu ajinunulie kagari kake alafu wewe uje umpangie mahali pa kukalaza? Ebo!
Alafu anatahadharisha tukio ambalo, nadra kutokea, kuliko matukio yanayotokea mara kwa mara kama gari yenyewe kupata ajari, ikiwa barabarani. Moto hata nyumba zetu tunazoishi hutokea.
 
Ni kwa nini usijenge kanyumba kako, uweke na kafensi ka kishikaji kabla ya kununua gari?

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
Ukijenga kanyumba na kuweka ka fensi, ajari ya moto hsitokei, mara ngapi umeshudia ajali ya moto, kuunguza vituo vya kuuza mafuta kuliko, ajari za moto kwenye nyumba za watu.

Sema raha ya gari kulaza kwako, hata kuwe na mvua kubwa utatoka, utaepuka garama za kulipia ulinzi, pia kwa wanaotoka usiku, inasaidia kukuepusha na wakabaji, na faida nyingi zingine.
Ila moto ni ajari popote hutokea.
 
TOKA NIZALIWE EARLY 90’s Ndani ya jiji la dar sijawahi sikia sheli iliyoungua na kuunguza magari.

Nikakumbuka Mwaka 2016 nilikua dalali wa magari, pale opposite na be foward zinapaki gari nyingi IT, with no risk.
Hizo sheli zinazounguza vigari ziko maeneo gani?

Nikajua utaandika risk ya kuibiwa
Oil com morogoro, mtampinga mleta mada Ila ukweli ndo huo, sheli sio sehemu salama Sana.
 
Oil com morogoro, mtampinga mleta mada Ila ukweli ndo huo, sheli sio sehemu salama Sana.
Yaani na wewe ilimradi tu uonekane umecomment. Lini sheli hiyo imeungua. Lini? Na oil com ya morogoro sehemu gani?
Taarifa uliona wap?
 
Back
Top Bottom