Mwanasayansi Kalivubha
JF-Expert Member
- Feb 4, 2024
- 344
- 926
UNAOJIFARIJI MBELENI WATABADILIKA WENGI WAO WATAENDELEA KUKUUMIZA BADALA YA KUBADILIKA.
Kuna usemi maarufu usemao kama huwezi kumpenda mtu vile alivyo sasa mwache na usijidanganye kumbadilisha awe utakavyo ndio umpende.
Huo msemo una maana pana hasa ukiwalenga watu ambao wanajifariji kuwa ipo siku watafanikiwa kuwabadilisha watu fulani wawe vile wakavyo kisha ndio wawapende , Hili zoezi ni ngumu sana japo kwa wachache huwa linafanikiwa
Kwanini ni zoezi ngumu? Zipo sababu kadhaa zinazofanya hilo zoezi liwe gumu kufanikiwa badala yake kupoteza tu muda,sababu hizo ni kama zifuatazo:
KAMA HUJAMPENDA ALIVYO SASA BASI HUYO SIYE WAKO, Kama unataka abadilike kwanza ndio umpende basi huyo sio wako bali unamlazimisha awe wako hivyo asipobadilika utajikuta umepoteza nguvu na muda na hajawa yule umtakaye.
WATU HAWAPENDI KUBADILISHWA; Mara nyingi watu hubadilika wenyewe tena wengine wakijua unawabadilisha ndio wanazidi kuongeza jinsi walivyo.
YAWEZEKANA NDIVYO ALIVYO : Yawezekana yeye ndio yupo hivyo sasa kazi kwako umpende ama umwache na ukiendelea kujidanganya kumbadilisha utajikuta unakuwa mshauri kila siku bila kufurahia mahusiano yenu ,wewe unakonda yeye ananenepa.
ACHIA WANAOENDANA NAYE, Sio lazima muendane na wewe, Dunia ina watu wengi ambao unaweza kuendana nao acha kumlazimisha awe huyo tu .
#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako