Unaomba kusamehewa madeni, halafu wewe unaongeza makato ya HESLB kutoka asilimia 8 mpaka 15

Unaomba kusamehewa madeni, halafu wewe unaongeza makato ya HESLB kutoka asilimia 8 mpaka 15

Huwa napata dakika chache sana za kutafakari watu kama ninyi lakini najiuliza kwann naumiza moyo na wajinga km ninyi?
Watu wasioweza hata kutofautisha L na R watakua na mawazo gani ya kujenga?? Ukiona hivyo jua elimu ya juu haimhusu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo

% ni liba au ni rejesho?
N kama ni lejesho nadhani unasaidiwa kumaliza deni lako haraka ili upumzike
Maisha hayapo hivyo, je mshahara wenyewe shilingi ngapi? Tusifanye mzaha kwenye maisha ya vijana wetu mnawasukumiza kwenye rushwa na vishawishi vingine kutokana na ugumu wa maisha yanayoletelezwa na makato hayo.
 
Watu wasioweza hata kutofautisha L na R watakua na mawazo gani ya kujenga?? Ukiona hivyo jua elimu ya juu haimhusu [emoji23][emoji23][emoji23]
Lakini dada L na R haiwezi kumfanya mtu ashindwe kutoa mawazo. Je kama alisoma english media ambayo hawafundishi kiswahili who knows.
 
Maisha hayapo hivyo, je mshahara wenyewe shilingi ngapi? Tusifanye mzaha kwenye maisha ya vijana wetu mnawasukumiza kwenye rushwa na vishawishi vingine kutokana na ugumu wa maisha yanayoletelezwa na makato hayo.
Lipa pesaaaaaaaaaaaa wewe
 
Lakini dada L na R haiwezi kumfanya mtu ashindwe kutoa mawazo. Je kama alisoma english media ambayo hawafundishi kiswahili who knows.
English Medium bado wana somo la kiswahili... na sio sababu ya kushindwa kutofautisha hizo herufi... !
 
Lipa pesa za watu wewe, kwani ulilazimishwa kuchukua mkopo. Kipindi wenzako wamekosa ulikua unawacheka umekosaaa
Akili yako ndio imeishia hapo?Hatujakataa kulipa,ila tunacholalamika ni kuongezewa kiwango cha makato tena ghafla tu!Acha roho mbaya,jiweke kwenye mazingira kama ni wewe!
 
Hiyo

% ni liba au ni rejesho?
N kama ni lejesho nadhani unasaidiwa kumaliza deni lako haraka ili upumzike
Vipi mchina nae akiongeza % za marejesho ili tumalize haraka ni sawa kwako tupunguze bajeti ya dawa ili tumlipe mchina ?
 
Inauma sana basi tu
Sema mtu mwenye mshahara mkubwa anaona kawaida au ambaye hakunufaika anaishia kubeza tu
 
Vipi mchina nae akiongeza % za marejesho ili tumalize haraka ni sawa kwako tupunguze bajeti ya dawa ili tumlipe mchina ?
Unadhani basi hayajui hayo?Anajua kabisa msingi wa hoja ila ni mfia chama na mtetezi wa serikali!
Huyu hata kesho serikali ikisema imepunguza hizo asilimia za marejesho,atakuja hapa kupongeza!
Ndivyo walivyo!
 
Ndugu walimu wenzangu na wanufaika wote waliosomeshwa kwa fedha ya serikali yaani BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU (HESLB),,, Juzi Jumatatu tarehe 28.12.2020 niliomba LOAN STATEMENT ya deni langu kutoka Bodi ya mikopo ili niweze kuclear deni baki ambalo kwa mujibu wa SALARY SLIP yangu ya 31.12.2020 Deni linasomeka Tsh. Mil 4.65,,
Aidha, cha kushangaza na kushtua jana HESLB wakanitumia kwa njia ya email statement ya deni langu ambapo Deni langu linasomeka nadaiwa Tsh. Mil 12.087 wakati kwenye Salary slip ya mwezi deni ni Tsh. Mil 4.65. Kiukweli nilichanganyikiwa nikawatumia ujumbe Bodi ya mikopo kuomba ufafanuzi wa hiki na leo Jumatano asbh nikajibiwa kuwa hakuna kilichokosewa kwenye statement waliyonitumia jana.
Baada ya kuona sielewi imelazimika nisafiri hadi Halmashauri kuonana na AFISA UTUMISHI ili aweze kunipa ufafanuzi wa jambo hili, nilipofika akampigia simu AFISA kutoka makao makuu ya HESLB ambaye ndo anashugulika na makato ya fedha zote kutoka kwa wanufaika wote nchini, alimpigia palepale mbele yangu na akaweka Loud speaker yule Afisa wa Bodi akaelez a mambo mengi sanaa kuhusiana na fedha hii. Ambapo kiujumla amesema kwamba watumishi wote tunaokatwa kupitia mishahara yetu deni tunaloliona kwenye hizo salary kama linapungua sio deni halisi bali deni la halisi analodaiwa mnufaika wanalo wao Bodi kwenye mfumo wao ambao mfumo wao hauna mahusiano yyte na Mfumo wa Lawson, hivyo deni letu halisi huwa haliwi updated kwenye salary slip ndo maana tunaona kila mwezi linapungua ila kiuhalisia ni hapana..
Akaendelea kusema mtumishi yyte akitaka ajue deni lake halisi analodaiwa basi aombe Loan Statement kutoka Bodi hapo ndo anaweza kujua deni lake halisi ambalo ni tofauti sanaaa na linaloonekana kwenye Salary slip zetu...
Akasema tena deni lililopo kwenye salary slip linapokwisha mtumishi anaweza akaona kama vile kamaliza deni, kumbe kuna deni kule bodi bado wanamdai. Hivyo akasema sasahv wapo kwenye mchakato wa kuandaa barua kuwatumia waajiri wote nchini madeni mapya ya wale wote ambao washakamilisha kulipa deni la kwenye salary slip ili makato yaendelee kama kawaida..
Mwisho Afisa huyo akamuomba Afisa Utumishi anipatie mimi namba ya huyo Afisa ili kama mahali nitakuwa sijamwelewa vzr niweze kumpigia wkt wwte kwa maelezo ya kina....
Hivyo ndug watumishi na walimu wenzangu ambao ni wahanga wa hili tusijipe matumaini ya kuclear hili deni tunaweza hata kustaafu nalo. Tupambaneni kutafuta hela ili watt wetu tuwanusuru na kuongia kweny hili janga la Bodi ya mikopo ili tuwasomeshe kwa fedha zetu hata kwa kujibana maana inauma sanaaa.
Yeyote atakayehitaji namba ya simu ya huyu Afisa kutoka HESLB kwa ajili ya maelezo ya ziada anaweza kunitafuta inbox nikamtumia. Asante

BY. MWL MUSSA A. IDDY
NAMONGE SEKONDARI
Wanaoshahikia CCM na hasa Magufuli,mimi huwa nawaona mentaly wana mapungufu.
 
Maisha hayapo hivyo, je mshahara wenyewe shilingi ngapi? Tusifanye mzaha kwenye maisha ya vijana wetu mnawasukumiza kwenye rushwa na vishawishi vingine kutokana na ugumu wa maisha yanayoletelezwa na makato hayo.
Hata kabla ya hayo makato, rushwa kwa wafanyakazi na ufisadi vilikuwa vikubwa sana, sasa sijaelewa wewe unamaanisha nini kwa hilo.
Swara la ufisadi na wizi ni 5abia ya mtu.
Kuna wafanyakazi wanalipwa zaidi.ya milioni kumi na tano lakini wanafaya ufisadi
 
Back
Top Bottom