Unaomba kusamehewa madeni, halafu wewe unaongeza makato ya HESLB kutoka asilimia 8 mpaka 15

Mabeberu weusi: angalia hiyo video

 
Wakati mnaandamana kudai boom halitoshi mlidhani mkopo ni zawadi?
 
Tumia akiri basi yeye kaomba kufutiwa au kupunguziwa na ninyi wafanya kazi.mliokopa ni wajibu wenu kuomba kupunguziwa au kufutiwa.

Pia swara na kupanda kwa makato ni la 2017 na sio 21 hivyo halina mantiki, kwani watu walishazoea,
Kama wanaona kuna shida basi nao watoe maombi watasikilizwa.
 
Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu!Tulipiga kelele sana wakati wa ongezeko la makato,hakuna aliyetusikia!Waliweka Pamba masikioni!
 
Bodi hawana takwimu halisi.wote mliomaliza madeni yenu ya Bodi nendeni pale ofisini kwao kila mtu anadaiwa.Yaani ni ajabu Sana hebu waulizeni aliyepeleka Deni kea mwajiri ni nani?je mwajiri alipata wapi Deni la mwajiriwa alipoanza kukata Hilo deni.msijipe matumaini kwamba mmemaliza madeni pale bodi madeni hayaishi.Mitano mingine

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Lakini dada L na R haiwezi kumfanya mtu ashindwe kutoa mawazo. Je kama alisoma english media ambayo hawafundishi kiswahili who knows.
English Media.........!!!!??? Hii nchi ina shida sana kwenye elimu.
 
Sijui wananchi wanalalamikia Nini, mbona nchi iko sawa tu
 
FAHAMU KIDOGO KUHUSU LOAN BOARD NA SHERIA MPYA

Code:
Bodi ya Mikopo imewanufaisha watanzania wengi sana ikiwa ni pamoja na kuwajengea watanzania misingi ya kielimu kwa ajili ya future katika maisha yao . Aidha, Asilimia 80 ya wanufaika wa mikopo ya bodi ni wale kina KAYUMBA Yaani watoto wa maskini. 

Sheria ya mwaka 2016 ya bodi ya mikopo iliyofanyiwa marekebisho ni sheria ANGAMIZI kwa watoto maskini.

Sheria imeweka wazi ( Watz wengi hawana tabia ya kujisomea) kuwa marejesho ya mkopo yatakuwa ni kwa 15%, na deni hilo litakuwa linaongezeka kila mwaka wa fedha kwa asilimia 6% ya deni halisi la mwanzo.

Kwa mfano.
Daktari ambae amesomeshwa na bodi, asilimia kubwa deni lao huwa kati ya mil 25 mpaka 30.

Basic salary yake ni 1.5 Mil 
Makato ya mshahara wake ni kama ifuatavyo, 

Helsb 225, 000 TSH
PAYE 295,090 TSH
NHIF 42,420 TSH
Pension. 80, 000

Total deduction 642, 510 TSH
take home yake ni 857,590 TSH —ana watoto na anasomesha! 
-----------------------------

Kwa sheria ya bodi ya mikopo, huyu bwana kwa mwaka ataweza kulipa 2.7Mil ( 225,000X12)

Hivyo katika deni lake la 30Mil , atakuwa amepunguza deni lake hadi 27, 300,000TSH ikifika mwisho wa mwaka wa fedha.

Mtu huyu atapaswa kuanza mwaka wa fedha mpya akiwa na deni la 27, 300, 000 TSH. 

Lakini sheria ya bodi inasema hapana, unatakiwa kuongezewa 6% ya 30 mil ambayo ni 1.8 Mil 

Hivyo deni analopaswa kuanza nalo ni 27,300,000+ 1.8 Mil sawa na 29, 100, 000 TSH.

Kwa mwaka unaofuata tena, atafanikiwa kuipunguza hiyo 29,100,000 Mil hadi 26,400,000 Mil na ndiyo ni kianzio cha deni lake kwa mwaka mpya uliofuata.

Sheria ya bodi itasema hapana, hii 26,400,000 lazima iwekwe 6% ya 30Mil ambaye ni 1.8 

Hivyo 26,400,000+ 1.8 mil 

Deni jipya kwa mwaka mpya uliofuata itakuwa ni 28,200,000Mil badala ya 26,400,000 and the list goes on. 

Yaani utakuwa unakwenda mbele na kurudi nyuma mpaka unastaafu.

Sheria ya mwaka 2016, inazidi kusema kuwa, ikiwa muhusika mpaka anastaafu, hajafanikiwa kumaliza deni lake, basi pension yake itafidiwa. 

Yaani, Ikiwa una pension ya 15 Mil , na deni lako lilibaki 20 Mil , Bodi itakula zote 15 Mil na itakudai 5 Mil na hiyo 5 mil itazidi kuongezeka kadiri miaka inavyokwenda mbele, ni hatari sana na mbaya zaidi watumishi wengi hawajui hii sheria. 

Ikitokea pension yako imeliwa yote na bodi,maana yake unazeeka ukiwa huna kitu.

I just can't figure it out , ni sheria kandamizi dhidi ya mtoto maskini iliyopitishwa na wabunge wetu tukufu. 

Ni kwamba mtoto wa maskini hatoweza kumaliza hili deni , ni deni la maisha hasa waliosoma makozi ya sayansi kama udaktari, Nesi, famasi , na injinia na wale waliosoma nje ya nchi.hawa wote madeni yao si chini ya 25Mil or so. It is a detrimental to these poor people, and Unfair. 

Mapendekezo 

1. Serikali ipitie upya hii sheria, na ifutilie mbali hiyo incremental ya 6% kwa kila mwaka, it is not even practical, watu wengi wanakufa na hayo madeni tena bado yakiwa makubwa mno. 

2. Irudishwe asilimia 8% au 10% badala ya 15% ya makato ya bodi, kwa sababu watumishi wa umma ndiyo wanufaika na hii mikopo, na wengi wanaangamia hali zao malikiti sokoni.

3. Bodi ya Mikopo itoe elimu maredioni juu ya utaratibu wa urejeshwaji wa haya makato WaTZ wengi haijui kitu kuhusu mambo ya sheria.

4. Sheria ya kuchukua pension ya watumishi walioitumikia serikali hadi kustaafu itolewe kwa Sababu ni mateso makubwa yatakuwa kwa hawa watu na hii ni jamii yetu inayoitumikia serikali ya Jamhuri miaka nenda rudi.

Watumishi wa umma wengi wanastaafu wakiwa maskini na fukara, uwachukulie tena hizo pesa za pension, kweli ? Doh tutapata laana katika nchi.

USHAURI.

1. Kwa wazazi ambao wanajiweza, achaneni na mambo ya kuwasukumizia watoto wenu kwenye mikopo mpaka muelewe vyema sheria ya marekebisho, hiki ni kilema cha maisha kwa wale ambao deni lao ni above 20Mil. 

2. Pia wahusika hakikisheni mnaipitia hii sheria na muelewe marejesho yake, you need to take precaution. Kama huelewi mtafute Mwanasheria akuelewesheni ni hatari sana fuatilieni haya mambo.

   ©️2020
 
Mambo yenyewe ndo Aya[emoji848]

Mwalimu anadaiwa billion 47
 
Hi serikali ni ya dhulma na uporaji mkubwa. Pole Sana mwalimu. Wafugaj wamepoteza mifugo yao kwa faini,wafanyabiashara wengi wanalalamika kodi zenye kupitiliza. Wavuvi walipigwa faini za kufa mtu.
 
This is the best time to prove that we can't exist on our own as a society we need leaders. At trying times like this it's when we sit back and review our values and process of selecting and vetting our leadership process. The best we can do is learn.

Vilaza ni changamoto kubwaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…