Unaona aibu kutamka bidhaa ipi mbele ya watu uwapo dukani?

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Kwa namna moja ama nyingine, kuna baadhi ya mahitaji yanatuwia ugumu kutamka kwa muuzaji mbele ya wateja wengine

Ukimuona mteja anakupisha uhudumiwe kwanza wewe, usidhani nia yake ni kukopa, wengine tumekuja kununua nyara hatari za kiserikali

Kwangu mie kutamka sentensi, "Mangi, nipatie wembe" mbele ya watu, huwa nafikiri watu wananichukulia mchafu. Huwa nahisi kuna kauli ya mteja inamjia kimya kimya ikimwambia "Anaenda kukwatua manyasi"

Pia kununua sabuni ya kipande usiku huwa naona soo, tena mbele ya wateja wengine inakuwa ngumu. Mara mia nitamke Condom

Unajihisi aibu kutamka bidhaa ipi ukiwa kwenye duka lililosheheni wateja?
 
Condom
 
......kuna hii ya kununua mipira ya kiume ni ishu, afu inakuaga kama mkosi wateja huwa hawatoki haraka hadi muuza duka anaanza kuhisi we ni mwizi......lakini pia kuna hii y a kuagizwa pedi na mpenzi nayo ni ngumu....kudeposit elf kumi bank na kudraw buku mpesa......
 
Nimefika kiduka fulani, nilitaka nikanunue maharage, hiyo ni jioni, nakuta mabinti wawili wazuri sijui wanafanya nini, unafanyaje? Nikauliza una tigopesa? Jamaa kasema hana, nikasema kama shujaa
[emoji23][emoji23]Aki, jumlisha na lile wenge. Yaani unakuwa sawa na mtu aliwekwa ndani ya jokofu
 
Nilikuwa naogopa kununua pedi. Hata sasa hivi naogopa ndiyo maana bora niende supermarket nikabebe tu .
Siogopi yaani sio shida zangu kabisaaaa. Asiyejua mimi ni mwanamke ni nani? 😅😅
 
Siogopi yaani sio shida zangu kabisaaaa. Asiyejua mimi ni mwanamke ni nani? [emoji28][emoji28]
Hahahaha umenikumbusha shoga angu mmoja ila yeye kakuzidi ujasiri. Anaenda kununua halafu haifungi wala nini. Atazunguka nayo atapita hata nyumbani kwako kukusalimia kaishikilia mkononi nakwambia.
 
Duh huyo balaa😅
 
Back
Top Bottom