Unaona kawaida kutangaza watu 518 wameuawa? Unasema utalibeba kwa utulivu? How?

Unaona kawaida kutangaza watu 518 wameuawa? Unasema utalibeba kwa utulivu? How?

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,505
Reaction score
40,002
Kwa mara ya kwanza tunaona kiongozi mkuu wa nchi akisimama hadharani na kuona idadi ya watanzania ambao amewatangaza kuwa wamekufa 518 na zaidi kwake anaona ni jambo la kawaida. Hashtuki!

Anapindua meza na kuwabebesha lawama waliouawa kuwa ilikuwa ni haki yao maana walibeba mabomu, bunduki mishale na vilipuzi.

Samia jambo ambalo hujui ni kuwa sisi wengine tulishuhudia kwa macho watu wakifyatuliwa risasi. Wengi walikuwa tu wamejikalia zao vijiweni tarehe 30 octoba kisha ilikuwa inakuja gari imeandikwa "Polisi" wanafyatua risasi kadhaa kisha wanatokomea.

Samia umetuona sisi ni wajinga sana? Kwamba unaweza kutudanganya na mambo yakaenda kama yalivyo? No! Utawajibika.

Au unahisi watu 518 uliowatangaza ni vifaranga vya kuku? Kwamba ni kawaida kabisa watu hao kuuawa na kisha kuwabebesha lawama?

Walioua ni jeshi la Polisi na wengi wao waliua tukiwashuhudia kwa macho. Kaa na hili.
 
Back
Top Bottom