Kwa starehe za kiwango cha kutisha kwa sasa mahali pake ni katika visiwa Maldives vilivyopo ndani ya Bahari ya Hindi huko Asia.
Haipo starehe ndani ya Ulimwengu huu utaikosa huko Maldives!
Matendo ya kishetani yatendekayo katika visiwa vile ni zaidi ya kusimuliwa.
Usichokijua Visiwa hivyo vipo kwenye hatari ya kumezwa na Bahari ndiyo maana watu wengi wa Mungu wanadai hiyo pengine ni adhabu fanani na ya Sodoma na Gumola.
Maelezo yako si ya kweli.
Maldives ni kisiwa maarufu kwa wale maharusi wapendao kufanya honeymoon za mbali, hivyo kwa wenzetu wazungu ambao hupanga harusi zao kwa muda mrefu, Maldives is top of agenda.
Pili, ukiingia Maldives viza yake wanakupa ya siku 30 kabisa ule maraha na ujishereheshe weye na mkeo mpya au mwenza au watu tu wapendao kufanya vekesheni za pamoja.
Wana hoteli za nguvu sana pale khasa ile iitwayo Hard Rock ambayo musiki wake hutokea kwenye swimming pool.
Je. wapenda Scuba weye? basi pale kuna kisiwa kingine kiitwacho Ari Atoll ambako kuna michezo ya Scuba Diving kwenye mawimbi.
Halafu, si kweli kwamba hiki kisiwa chaelekea kuzama bali ndivyo kilivyoundwa kuelea juu ya maji (floating) hivyo maji yake ya blue, mchanga mweupe na miti ya minazi ni burudani tosha pale upepo mwanana unapokupiga usoni kisha ukalala usingizi wa pono.
Hivyo basi Maldives ( maana yake visiwa vya Maldive) ni visiwa vya joto la kitropiki ambavo vimesheni mahoteli na sehemu kadha wa kadha za kura raha.
Kwenye usalama wenyewe wanashauri baada ya kupata viza una budi kupakua app ya kukufuatilia endapo utapotea au kupata tatizo yaitwa TraceEkee ambayo yapatikana kwenye AppStore.
Lakini starehe za kutisha hazikosekani mahali popote na Maldives kuingia watakiwa uwe na mfuko ulojaa khasa ili uweze kufaidi.