Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Kutongoza ni mchakato wa kujuana.
Ni kitendo cha kuruhusu nyie wawili mjuane zaidi. Ndio maana hautakiwi kuacha kumtongoza mwanamke wako. Hata kama mna miaka mingapi pamoja.
Mchakato unaohusisha;
Kujuana historia zenu,
Kupata muda pamoja,
Kufurahi pamoja,
Kuchombezana,
Kufanya mapenzi, na
Kujua mwenzio anapenda/ hapendi nini.
Ukifanikisha hayo, utafurahia mahusiano mpaka hutoamini.
Kujuana huko hakuishi.
Sababu sisi wenyewe tunabadilika. Tunakua pia.
Ndo maana inabidi usimwambie mwanamke kila kitu mapema. Naye huwa hakuambii kila kitu.
Bali kadri muda unavyokwenda unamjua huyu yupo hivi na hivi.
Hivyo, usiwe na wasi wasi kumfata mwanamke kutaka kumjua.
Ukijiwekea akilini kwamba “namfata ili nimpe nafasi ya kujuana”. Hautoona ni jambo gumu.
Utakua umejitua mzigo kwamba inabidi umshawishi sana.
Ila unajua kuwa inabidi mshawishiane. Kila mtu aweke nguvu kwenye kujuana.
Kwaiyo unamfata ile umpe nafasi mjuane. Sio kumshawishi ili akupende sekunde hiyo hiyo.
Tongoza ukiwa unajua una muda, tongoza bila presha ya kutaka kumshawishi saaana, tongoza ukijua hata kama huna maneno mazuri sana una nafasi ya kujuana.
Usijitese utamshawishije leo/ sasahivi mana una miezi mingi mbele ya kujuana.
Haimaanishi usichukue hatua/ uache kusongesha mambo mbele, hapana, namaanisha usiwe na haraka sana mpaka hujui cha kufanya.
Lakini pia usiwe taratibu sana ukaishia kuwa rafiki.
Japo dakika za mwanzo (mkikutana) inabidi uweke nguvu ili naye aweze kuanza kuweka nguvu sababu hakujui na wewe ndo umemfata.
Kwa mwanamke aliyevutiwa sana na wewe hautokua na haja ya kufanya hivyo. Sababu naye atakua anaweka nguvu zake, pengine hata zaidi yako.
Ikifika siku mkasema tunajuana, ujue ndo mmeanza kuzoeana.
Mtaishi kama ndugu au kaka na dada ndani.
Au mwanamke akionesha anakujua ujue kuanzia hapo hutomwelewa. Atakua haeleweki kwako. Na penzi halitakua na raha au hutopata kabisa.
Sababu tukishakijua kitu hakina umuhimu tena kwetu kukiwekea nguvu.
Ila kama bado hatukijui kitu tunachokipenda tutaendelea kuwa nacho karibu na kukiwekea nguvu.