Unapendekeza gari ipi kati ya IST, Runx, Ractis au Allex?

Unapendekeza gari ipi kati ya IST, Runx, Ractis au Allex?

Sema haya mawazo ya kimaskini sana eti consumption ya mafuta ikufanye umiliki kitu usichokipenda
 
Wakuu naomba mnipe mawazo kidogo kati ya hizi gari ipi itafaa kwa mizunguko ya mjini tu, ukizingatia muonekano na ulaji wa mafuta
Mleta mada,

Nakusalimu.

Kama mdau aliyetangulia ku-comment / reply hapo juu yaani Zanzibar-ASP kuhusiana na suala la muonekano.

Kwa mfano, binafsi hua naona Ist, inawapendeza sana wanawake zaidi ya wanaume, na Allex / Runx inawapendeza sana wanaume kuliko wanawake.

Kiuhalisia, hua tunaangalia mambo yafuatayo :

1. Budget
2. Uimara wa chombo
3. Gharama za kila siku kukihudumia chombo
4. Upatikanaji wa vipuri na bei zake

Hayo ndio ya msingi, na muonekano wa gari uitakayo itategemeana sana na namba moja yaani budget yako.

Utumiaji wa mafuta , kwa gari zote mbili
Yaani Ist ya around 2003 na runx ya around 2004 ni sawa.

About 16km/L

Runx ya 1,490CC ina power na inatumia mafuta sawa na Ist ya 1,290cc ambayo kiuhalisia haina power kubwa sana.

Bei pia zimetofautiana kidogo. Runx / Allex iko juu zaidi ya Ist.

Body na mafundi,
Naona Allex ni ngumu zaidi ukilinganisha na Ist,maana ni Corolla ile.

Mafundi, wengi wanazimudu vizuri zote mbili bila tatizo, na hata spare parts zake ni nyingi vile vile.

Otherwise, jiongeze kidogo, fikiria BMW 3 series around 13.8mil
 
Brother,

Hii ni gari moja, sema wametofautisha tu majina.

Yaani the earlier model (allex) was simply tweaked kidoogo.

Kwahiyo toyota modified the back storage compartment with an upward-swinging door.
Ndipo sasa the new modifications ikaleta the birth of Corolla FX hatchback; ambayo was later assigned na a new brand name, yaani Runx
Nafahamu hilo ni kama probox na succeed ni gari moja ila kuna utofauti kidogo
 
Mzee IST zipo Cc 1290 na 1490 tuu
Na Runx zipo za 1490 tuu
Runx zipo za 1800cc pia ambazo zimegawanyika makundi mawili. Kuna zenye injini ya 1ZZ-FE for economy, na zenye 2ZZ-GE for performance.
 
Zote hizo ni takataka!
Huu ndo uzuri wa Jamiiforums. Kuna yadi ya kuuza magari pale morocco, ukiwa mataa kuelekea mwenge, kama mita 70 tu upande wa kulia kuna bango. Na kuna barabara inaelekea kulia, ukipinda pale mita 30 hivi ndipo yadi ilipo.
Nilicho washangaa wale wahindi, pamoja na kuuza magari ya aina mbalimbali, eti walikua wanatembelea takataka IST.
 
Sema haya mawazo ya kimaskini sana eti consumption ya mafuta ikufanye umiliki kitu usichokipenda
Kila mtu ajikune anapofikinia, sasa hata akiipenda BUGAT, wakati hana uwezo wa kuinunua si atakua mpumbavu.
 
Gari zote ulizotaja zinakuja na option mbali mbali za engine. Kuna zenye 1.3L, 1.5L na 1.8L utachagua mwenyewe kulingana na mahitaji yako.
 
Wakuu naomba mnipe mawazo kidogo kati ya hizi gari ipi itafaa kwa mizunguko ya mjini tu, ukizingatia muonekano na ulaji wa mafuta
Leo ndio naiona hii thread yangu. Ngoja nitoe mrejesho, kwanza nashukuru sana kwa ushauri wenu wakuu ulinisaidia sana katika kuniongoza kuchagua gari sahihi kwa matumizi yangu kipindi hicho.

Niliupokea ushauri wenu nikauchakata kwa kuzingatia mahitaji yangu niliamua kununua RUN X, kwa kweli ni gari nzuri sanaa na niliifurahia sana ukizingatia ndio ilikua gari yangu ya kwanza kuimiliki. Ingawa baadae nilikuja kuiuza mwaka 2023 na kuhamia kwenye Subaru Forester. Ila ni moja ya gari ndogo nzuri sana, i recomend kwa any first time car owner kuiconsider Run x hatojutia.
 
Back
Top Bottom