Wakuu naomba mnipe mawazo kidogo kati ya hizi gari ipi itafaa kwa mizunguko ya mjini tu, ukizingatia muonekano na ulaji wa mafuta
Mleta mada,
Nakusalimu.
Kama mdau aliyetangulia ku-comment / reply hapo juu yaani
Zanzibar-ASP kuhusiana na suala la muonekano.
Kwa mfano, binafsi hua naona Ist, inawapendeza sana wanawake zaidi ya wanaume, na Allex / Runx inawapendeza sana wanaume kuliko wanawake.
Kiuhalisia, hua tunaangalia mambo yafuatayo :
1. Budget
2. Uimara wa chombo
3. Gharama za kila siku kukihudumia chombo
4. Upatikanaji wa vipuri na bei zake
Hayo ndio ya msingi, na muonekano wa gari uitakayo itategemeana sana na namba moja yaani budget yako.
Utumiaji wa mafuta , kwa gari zote mbili
Yaani Ist ya around 2003 na runx ya around 2004 ni sawa.
About 16km/L
Runx ya 1,490CC ina power na inatumia mafuta sawa na Ist ya 1,290cc ambayo kiuhalisia haina power kubwa sana.
Bei pia zimetofautiana kidogo. Runx / Allex iko juu zaidi ya Ist.
Body na mafundi,
Naona Allex ni ngumu zaidi ukilinganisha na Ist,maana ni Corolla ile.
Mafundi, wengi wanazimudu vizuri zote mbili bila tatizo, na hata spare parts zake ni nyingi vile vile.
Otherwise, jiongeze kidogo, fikiria BMW 3 series around 13.8mil