Half american
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 46,410
- 114,823
Habari zenu wakuu. Poleni sana kwa yote tuliyopitia na tunayoendelea kupitia ndani ya taifa letu.
Wakuu, ukiwa katika mchakato wa kuoa/kuolewa (engagement, send off& kufunga/kubariki ndoa) jitahidi sana kuwa na utulivu na muaminifu. Hiki ndio kipindi muhimu sana kuelekea kufanikisha safari ya upendo kati ya wapendanao. Usimpe mwenza wako sababu ya kukuona hustahili.
Inasikitisha sana kuona mtu anachangia mwenyewe kuitia doa na kufelisha mchakato huo kwa kukosa utulivu na uaminifu.
Unajua unaolewa umeshavishwa pete tulia, mnazitia aibu na doa familia zenu. Mnawapa kataa ndoa ushindi mapema kabisa.
•Acha kuendekeza mazoea na mawasiliano yasiyo na mipaka. Hasa maofisini.
•Achana na ma ex watakuharibia na hawana la kupoteza.
• Achana na huyo mzazi mwenzako anaekupotosha wakati yeye kaoa/kaolewa au hana mpango huo.
•Acha tamaa ridhika na ulienae na uwezo wake.
Kuanza kurudi rudi nyuma kutakugharimu na utabaki na majuto maisha yako yote. Kumbuka hakuna anaependa kuwa na mtu asie muaminifu hata kama yeye ni muhuni.
Inasikitisha sana na ni aibu watu wamejitoa mpaka send off tayari alafu linatokea fumanizi na habari inaishia hapo, kuanza kusumbua watu wakuombee msamaa kwa jambo ambalo linawezekana kulizuia. Aibu nyingine zinaepukika wakuu.
NB: Kama hakuna muaminifu, kuwa muaminifu. Uhuni sio dili.
NAWASILISHA