stabilityman
JF-Expert Member
- Jul 9, 2024
- 857
- 1,810
Sawa kiongozi, tumekusikia 🤝nyumba kwa ghalama naafuu
ujue unaongeza ghalama
Ujenzi ni grama ... Kizuri hugharimu na kuzingatiwa kwa ukaribuEleza gharama za kujenga kila nyumba uliyotuletea - Standard estimates.
Kwa kweli.Kwa kweli kama hela ipo na ninataka space kubwa kwa kila kitu why not?
Jiko kubwa na choo cha nafasi ndio napenda
Ungetoa ushauri ila usitusemee eti ya nini
Ila wataupokea ushauri wako wenye bajeti ndogo
Kwa kweli.
Sisi wengine tunapenda nyumba zenye nafasi sio tupishane sebuleni kwenye viti kupita kwenda jikoni.
Hapana kwa kweli.
I Need spacious house.
iwe tu kubwa nipite kwa kujimwaya mwaya!
Jikoni kuwe na nafasi nje kuwe na nafsi chumba kiwe na nafasi jiko liwe na nafasi kwa ujumla ni nafasi tu kubwa aiseeh!
Wenye bajeti ndogo za ujenzi sawa, ila na wanaofikiria ujenzi wa udogo.
Sisi wa big big everywhre big atuache kidogo.
Yani we ni mimi!Kwanza kabla ya kujenga naangalia ukubwa wa kiwanja at least kianzie hata 600 mpaka 800
Jiko la watoto kujimwagia uji sitaki
Nataka mama ajiachie
Choo hata ukianguka chance ya kuvunjika au kipiga kichwa kwenye ukuta ni mdogo Kama ni kikubwa au sio?
Choo kama banda la kuku hapana
Kumbe ndiye huyu?Fundi njaa unayelilia 300/ kwa mwezi hutaki kijana wako apewe
Bora nikutumie hela uanze kutujengea tu kwa kweli 😂😂Yani we ni mimi!
Nijenge nyumba bila kuwa na uwanja wa kupokelea mahari sio kweli!
Nijenge nyumba bila chumba kikubwa cha kulala niweze kupanda na kushuka kitandani kutokea upande wowote,sio kweli
Nijenge nyumba bila jiko kubwa ambalo baba watoto akikataka kunikumbatia mpk aniite chumbani , sio kweli
Kwa ujumla nyumba tu iwe kubwa jamani!
Mambo kufungua mlango wa choo unagonga sinki la choo, hapana aisee.