Unapokutana na hali ya usaliti (Snitch) Ughaibuni ufanye nini?

Unapokutana na hali ya usaliti (Snitch) Ughaibuni ufanye nini?

real hustler

Senior Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
143
Reaction score
204
Habari za masiku tena, mwana JF.

Mara nyingi, tuwapo hapa Tanzania, tunaamini wengi wetu waliopo nchi zilizoendelea, i.e. Europe au U.S.A., wameshaagana na matatizo; kazi yao ni kuokota tu vibunda.

Sasa, ninaye rafiki yangu ambaye alipata nafasi ya kwenda U.S.A. kimasomo. Akiwa huko, amekutana na Watanzania wengine wawili, na wote wanaishi katika apartment ya pamoja. Rafiki yangu huyu si muongeaji sana kiasili, lakini anasema miongoni mwa Watanzania hao, mmoja ni kama cherehani – yaani, haachi kuongea na hilo limekuwa changamoto kwake mno. Kibaya zaidi, yeye ndiye amepewa jukumu la kuwafahamisha wasimamizi (supervisors) kuhusu chochote kinachoendelea katika apartment, na hivyo inamlazimu kushughulika na Watanzania wenzake.

Pia, anasema kuwa kila anapojaribu kutoka jioni kwenda kutafuta mishemishe (kazi) mtaani, huyo mwenzake anamripoti kwa wasimamizi kuwa anafanya kazi. Kumbuka, kulingana na mkataba wa program, hairuhusiwi kufanya kazi na anaweza kurudishwa Tanzania. Hata hivyo, kuna watu wengi kutoka Asia wanafanya kazi bila shida yoyote, na ndio walimuunganisha na kazi hiyo ya mtaani. Anasema hali nyumbani si nzuri kiuchumi, kwani ameenda huko kwa ufadhili tu, na anahitaji ajichanganye kwa kazi za mtaani ili aweze kusaidia familia huku Tanzania na kuongeza akiba yake kwa ajili ya nyumba (Tanzania).

Tatizo ni kwamba huyo roommate Mtanzania amekuwa kikwazo kikubwa kwake katika safari yake hiyo.

Kaniomba ushauri, na nikamwambia ajitahidi kuwa mbali na huyo snitch Mtanzania.

Kama ungekuwa wewe, ungeishije na mtu kama huyo katika nchi za watu, huku ukiwa umeenda kutafuta maisha?

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom