Unapolalamika mgao wa umeme jiulize wewe una miti mingapi kwako ya kuvuta mvua ili mito isikauke na kupata umeme?

Unapolalamika mgao wa umeme jiulize wewe una miti mingapi kwako ya kuvuta mvua ili mito isikauke na kupata umeme?

Kyambamasimbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
762
Reaction score
1,597
Ifike mahali sio kitu Ni kulaumu Serikali na kusahau kwamba wewe ndie muuaji maarufu wa miti na zaidi unakuta kwako hauna mti hata mmoja. Tubadilike mama Samia haleti mvua bali tutunze mazingira tutunze asili sio kuangamiza miti na kuamini kuwa ni uchafu.
 
Nimetoka kuongea na mama yangu sasa hivi, at wametoka kulilia maombini mvua inyeshe. Nimesema tuwe tunakumbuka na namna tunavyokata miti ovyo siku hizi, ili tujenge, mkaa, kuni...mbao nk.
 
Mkuu, wakapande kwanza miti hao waliokuwa wanatoa tenda za kuuza magogo nchi za nje....halafu ndio uje na huu upuuzi.
 
Nimetoka kuongea na mama angu sasa ivi,at wametoka kulilia maombini mvua inyeshe... Nimesema tuwe tunakumbuka na namna tunavyokata miti ovyo sikuhizi....ili tujenge,mkaa,kuni...mbao nk...
Hongera Sana To yeye from Green city
 
Mkuu punguza ugasho na umbea.

Watanzania wanataka umeme wa uhakika si hoja dhaifu unaleta mbele ya kadamnasi.

Watu kama wewe ni wakutandikwa bakora.

Serikali dhaifu inachukua kodi, mikopo, misaada, lakini hakuna cha maana sana wanafanya badala yake wanamsingizia mwananchi masikini eti aakata miti ndiyo sababu tunakosa umeme.

Sababu yakukosa umeme au maji Tz ni wizi, uzembe, kukosa ubunifu na tamaa kwa wanaojiita serikali.

Fungua macho, kama unataka kuona utaona.
 
Aaaaaaah sio gesi ya Mtwara tena, tuliambiwa wamakonde wakikubali bomba likajengwa tutakuwa na umeme hadi tutauza nje, sasa inakuwaje tena tunaanza kulaumiana kuhusu miti
 
Back
Top Bottom