Unapolipa deni kumbuka haya (M-pesa, Tigopesa, Halopesa nk)

Mi nikikopa kwa mtu hua napiga hesabu ya pesa aliyokatwa wakati ananitumia, pesa atakayotolea na pesa nyingine ya soda ili siku nikikwama asisite kunikopesha.
Ukifanya hivi huwezi kugombana na watu.
Ingawa inaumiza kwa gharama lakini hakuna namna.
 
Ukilipwa hata bila ya kutolea wewe shukuru maana siku hizi kulipa deni ni mtihani kweli kweli.
 
Mkuu kutuma pesa kwenye mtandao hasara huwa haikwepeki ni bora kupata hasara ya makato kuliko kupata hasara mara mbili ya makato na yakutolea
Tanzania nchi yetu, ina Mambo ya ajabu sana, tunapenda vitu vya ajabu ajabu hatutumiii bank ambazo ni chipu na tunafata simu ambazo ni expensive
 
Kwani ndugu zanguni tatizo NI kiasi ulichonikopesha au ile Ada ya kutuma na kutolea??Kama NI pesa ya kutolea basi nikopeshe Kwanza laki Tano then muda wa kulipa niwe nakutumia ile ya kutolea kwanza
 
Kama ni pisi Kali, namkopesha tena kiroho safi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…