Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Tonge lipo mdomoni na pengine hata umeanza kulimega na kulitafuna polepole na pale anapozuka mtu kutoka kusikojulikana na kukunyang'anya unajisikiaje haswa pale ambapo unajaribu kuling'ang'ania lakini linateleza na mwingine kwa kasi ya ajabu analitumbukiza mdomoni kwake na kulimeza kwa mkupuo mmoja..............hata halitafuni........hivihivi na wewe unaona...................hivi unajisikiaje......unapigana............unatusi..........unajilaumu kwa nini ulichelea kulimeza?.........maana aliyelimeza anakutambia............kuwa ni uzembe wako.......kwa nini ulizubaa kulimeza ukabakia unalimega tonge la watu polepole..........huku ukidhani kwa vile unalimega ni la kwako.....yeye adai ana njaa na ndiyo maana hakulichelewesha...........akalimeza na huku hana mashaka ya tonge kumkwama kooni na hata kama likimkwama ni matunda ya kuzima kiu ya njaa kali aliyokuwa nayo......mezeni matonge yenu msije mkalizwa...................acheni kuahirisha maamuzi hadi siku mjanja akazuka na kukunyang'anya tonge lako..................lol.............na kukuachia maumivu yasiyo na tiba au hata kupoozwa..........
nasaha zenu zahitajika....
nasaha zenu zahitajika....