Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Pale ambapo mtu ana taarifa ya mapema kwamba , mumewe au mkewe anazini na Fulani, kisha akajiandaa kwa silaha na kuwavizia wahusika halafua akawafumania na kumuua mmoja au wote, sheria inambana mfumaniaji. Sheria ina huruma pale tu ambapo mfumaniaji hakuwa kabisa na muda wa kutafakari kuhusu tukio.
Kisheria fumanizi ni aina ya udhalilishwaji wa kimatendo ambapo mtu anamkuta mkewe au mumewe akiwa anataka, anafanya au amekwishafanya tendo la ndoa na mtu mwingine. Kisheria, ili kitendo cha fumanizi kipelekee kwenye udhalilishaji yapaswa kuwe na hasira kali, zinazotokana na udhalilishwaji wa ghafla na kusiwe na nafasi ya hasira hizo kutulia.
Pale ambapo mfumaniaji anaingia chumbani mwake bila kuwa na hili wal lile akamkuta mkewe akiwa kitandani na mwanaume mwingine, kama mfumaniaji ana kisu kiunoni akakichomoa na kumuua mgoni wake. Hapa mfumaniaji sheria inamlinda. Lakini kama aliwakuta hivyo chumbani kisha akaenda jikoni kutafuta kisu na kuja kumchoma mgoni wake. Hapo ni kosa la moja kwa moja. Hii ni kwa sababu kuna nafasi kati ya tukio na uamuzi wake.