Unapovizia kufumania na kuua basi jua imekula kwako!

Unapovizia kufumania na kuua basi jua imekula kwako!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421


Pale ambapo mtu ana taarifa ya mapema kwamba , mumewe au mkewe anazini na Fulani, kisha akajiandaa kwa silaha na kuwavizia wahusika halafua akawafumania na kumuua mmoja au wote, sheria inambana mfumaniaji. Sheria ina huruma pale tu ambapo mfumaniaji hakuwa kabisa na muda wa kutafakari kuhusu tukio.


Kisheria fumanizi ni aina ya udhalilishwaji wa kimatendo ambapo mtu anamkuta mkewe au mumewe akiwa anataka, anafanya au amekwishafanya tendo la ndoa na mtu mwingine. Kisheria, ili kitendo cha fumanizi kipelekee kwenye udhalilishaji yapaswa kuwe na hasira kali, zinazotokana na udhalilishwaji wa ghafla na kusiwe na nafasi ya hasira hizo kutulia.


Pale ambapo mfumaniaji anaingia chumbani mwake bila kuwa na hili wal lile akamkuta mkewe akiwa kitandani na mwanaume mwingine, kama mfumaniaji ana kisu kiunoni akakichomoa na kumuua mgoni wake. Hapa mfumaniaji sheria inamlinda. Lakini kama aliwakuta hivyo chumbani kisha akaenda jikoni kutafuta kisu na kuja kumchoma mgoni wake. Hapo ni kosa la moja kwa moja. Hii ni kwa sababu kuna nafasi kati ya tukio na uamuzi wake.

 
Mara nyingi hawawezi pata uhakika kwamba ulijiandaa...unless ulimwambia mtu...ulienda na silaha ambayo usingetakiwa kuwa nayo katika mazingira ya kawaida au ukubali mwenyewe.
 
Sisi tulio kama Juliasi Kaizari wala hatuna hata haja ya kufumania!
 
Hata ukifumania huna haja ya kuua,maisha bado yatazidi kuendelea tu.
 
Heee mwenzetu unajiandaa na fumanizi au vipi?
 
kumbe bora kutembea na bunduki masaa 24..lol

unashuti kwanza ,halafu ndo unauliza maswali lol
 
ina maana nikienda kufumania guest au hotel imekula kwangu kwani nilijua wapo mule si kushtukiza!naona ni bora kuwa na mtego wa mganga wa kienyeji akijaribu kubeep na ninihino zisiachane
 
Back
Top Bottom