lup
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 2,514
- 2,741
Za mda huu wadau JFGT, naamini mko vizuri na siku mnaimalizia kwa amani
Niende kwenye mada;
Katika utafutaji wa maisha hasa pale unapoamua kujikwamua kimaisha na hali bado uko chini sana na haujui utaanzaaje hata kama una mawazo mengi ya kuanzisha jambo/kitu au mrandi fulani.
Mara zote unapokuwa na maisha magumu na hauna nyenzo au mtaji kwa ukweli huwa kuna kuwa mawazo mengi sana ya nini cha kufanya na tatizo huwa ni mtaji tu, mfano leo unaweza ukawaza, nikipata hata elfu hamsini tu naweza hata uza maembe na kwenye akili yako unaona kabisa kuna site (sehem)nzuri ya kuuzia maembe na hadi faida yake.
Lakini kesho tu unaweza unapata wazo lingine nzuri zaidi tena lenye mtaji kidogo sana, lakini kabla ya kufanikisha mawazo mawili tayari yanakuja mengine na mengine mengi.
Hivyo kujikuta mnakuwa na mipango na malengo mengi ambayo kiuhalisia hakuna hata moja ambalo limeanza kutekelezeka.
Lakini pia unaweza ukaanza jambo au mradi fulani halafu kabla ya kufika popote au ukapata changamoto fulani lakini ghafla unaona wazo au mradi huo haufai na unaanza mwingine tena na usipoangali inakuwa ndio tabia yako huku umesahau mda na gharama vinaenda.
Ukweli ni kuwa hakuna kitu chochote ambacho hakina chagamoto lakini kumbuka kila kitu ukikifanya kwa moyo na makusudi ya kushinda lazima utaona matokeo yake.
Kwa nini nimesema tuwe na tabia ya Simba au kwa nini tujifunze kwa Simba?
Simba anapokuwa kwenye mawindo pale anapokuwa ameamua kufatilia mfano pundamilia fulani, kiukweli huwa hapindishi wazo lake hata kama atatokea pundamilia mwingine karibu na awe amenona kiasi gani lakini bado atamuacha na atamfuta yule wa mbali bila kujali pundamilia huyo yupo umbali gani na ana nguvu kiasi gani.
WEKEZA PALE MOYO WAKO UNAKUPA KUPENDA NA UNAAMINI KUWA HAPO NI LAZIMA UTATOKA TU!