Kwani kila unachoshauriwa na mkeo lazima ukubali? wewe si mtu mzima bwana? nawaheshimu sana akina mama kama kweli umefanya chaguo zuri na kuoa mwanamke anayeifaa kuwa mama ya watoto wako. Kwanza nina mifano mingi tu ya wanawake ambao waume zao walikuwa kwenye position nzuri tu lkn wakajisahau na starehe, lkn mwanamke ndiye aliyebana pesa na kwenda kununua shamba ambalo leo hii baada ya mwanaume kustaafu ndo wamejenga hapo na haishi kumsifia mke wake kwamba bila mama watoto sijui angefanyaje. Kama ulikutana na mkeo Baa, Club au kwenye starehe nyingine na wewe uka pledge ku mantain zile starehe hakika utashangaa maisha haya. Ndio mwanamke ni binadamu ana mapungufu yake hata sisi wanaume kuna mambo tunayafanya bila kushirikisha wake zetu na yana cost sana family zetu. Mfano hii hii concept ya kukataa kushauriwa na mwanamke ilinifanya nikose mambo mazuri mengi tu. Wakati tupo wachumba, mimi nilikuwa nafanya kazi na napiga kitabu, bado nilikuwa nakaa kwa kaka yangu yeye akikaa kwa maza wake mdogo. alinipeleka kimara kule kulikuwa na mashamba wakati ule 2002 yalikuwa yakiuzwaelfu hamsini, mimi nikaona aaagh mwanamke huyu ananishauri nini tena hivi watu wakisikia eti mwanamke kanipeleka kununua kiwanja si watasema jamaa katawaliwa, sikununua. Akaniambia tuwekeze pesa kidogo kidogo tununue friji kubwa, nikona huyu mwanamke mbona anataka kunitawala? sikumsikiliza. baadaye sana nimeshaoa ndo nakumbuka sasa eti vile viwanja vipo miaka ishapita hapo ananiambia si ulidhani nakushauri vibaya. Toka hapo nikajifunza, nikiambiwa kitu tunakaa chini tunajadili tunabisha tunagombana mwishowe tukifikia muafaka namwambia fuatilia au ngoja nifuatilie au twende wote tufuatilie mwishowe tunaamua kitu cha msingi. Najua kuna tofauti sana kati ya mwanamke na mwanamke lkn mimi wa kwangu wa jamani nampa mia.