Unasikiaga wanasema hakuna aijuaye kesho, si kweli. Nioneshe hivi vitu vitatu na mimi nitakuonesha kesho yako

Unasikiaga wanasema hakuna aijuaye kesho, si kweli. Nioneshe hivi vitu vitatu na mimi nitakuonesha kesho yako

NANGA WA DEPO

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
917
Reaction score
1,201
1. Nioneshe vitu unafuatilia mara nyingi mitandaoni au page unazo-follow (Insta, Facebook, WhasApp, TikTok n.k.)

2. Nioneshe marafiki zako angalau watano tu.

3. Nioneshe ratiba yako ndani masaa 24 ya siku
 
Mm marafiki watano mbali, ukinambia nikuonyeshe mmoja sina, labda useme nikuonyeshe watu ninaofahamiana na kufanya naonkazi
 
Ukiachilia mbali huo mtazamo wako je unajua kesho utaamka au huamki? Hata litakalo tokea baadae hulijui
 
"Hakuna aijuaye kesho". Tafsiri yake ni kwamba hakuna anayejua tukio/shida/jambo litakalompata sekunde/dakika/saa/siku zijazo. Yani hakuna anayejua hali yako kiuchumi/kiafya itakuaje Kwa muda ujao.
Hilo lipo mikononi mwa mwenyezi MUNGU.
 
Huijui kesho kwa sababu kesho haifiki.

Kesho itaendelea kuwa kesho.
 
Unataka kuleta ngonjera za motivation speaker??

Hii ni kama ile unaambiwa kula vizuri,fanya mazoezi,pumzisha mwili wako.halafu unakufa kwa ajali

Unawezapewa mpaka salio la acc na kesho mtu husika akaamka hana hata 100😁😁.
 
Back
Top Bottom