Unasoma ILI IWEJE?

Unasoma ILI IWEJE?

Nakuelewa vizuri sana! Kwa mtazamo wangu, elimu yetu inatufundisha woga wa maisha badala ya kutufungua na kutuwezesha kukabiliana na changamoto za kila siku maishani.

Mfano mdogo tu, mtu mwenye elimu ya kawaida yuko ki halisia zaidi (more practical) kuliko mtu mwenye shule kubwa japo sio wote. Laiti tungepewa mtihani wa kuulizwa na watoto umefanya nini leo kazini, kuna watu wangeshundwa kujibu licha ya kwamba kila siku wanaenda kazini na wanalipwa mishahara mikubwa. Nasema watoto ili uweze kumweleza akuelewe unachokifanya kwa sababu mtu mzima ata jifanya amekuelewa hata kama kimsingi hujamshawishi kile unachokifanya unapokua kazini.

Mathalani, ma cashier kwenye ma benki wangelipwa pesa nyingi kwa sababu kazi yao inatambulika na kila mtu kuanzia aliyeenda shule hadi asiyejua kusoma. Kuna watu watakwambia sijui strategies, hawezi quantify kwa siku amefanya kitu gani tangible lakini mishahara ndio hiyo lumbesa.

Ndio maana tumekua na vijana wanaotafuta namna ya kupata mishahara mikubwa bila ya kujali kama watakua na uwezo wa kuzifanya hizo kazi zenyewe, mwisho wa siku ni frustration kibao.

Elimu ni nzuri sana kama itatafutwa kwa lengo la kuongeza uwezo na maarifa ya kukupatia ujasiri na maarifa ya kutatua matatizo yako na yanayoizunguka jamii kwa ujumla.

Nafurahi kuwa Jf na member kama wewe!
Kuna linalo weza kufanyika kufanya elimu yetu more practical?
Cc mpigamsuli
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi kuwa Jf na member kama wewe!
Kuna linalo weza kufanyika kufanya elimu yetu more practical?
Cc mpigamsuli

Tungeacha vile vitu ambavyo hatuna uwezo navyo kwa hao waliovianzisha au wenye uwezo navyo. Sisi elimu yetu ikajikita kwenye kilimo na ufugaji, ikiwezekana na mambo ya ujasiriamali. Hapo hata tusingekua na mjadala wa tutumie kiswahili au kiingereza kufundishia, tungetumia kiswahili tu kwa sababu kila kitu kipo wazi.

Mambo ya electronic, sijui nyuklia tuwaachie haohao, tukihitaji hizo huduma tuta nunua kutoka kwao. Nilishawahi kusema na leo narudia tena, tuna akili sana sema tu hatujajua namna ya kuziwekeza kwenye maeneo stahiki tukafaidi matunda yake. Elimu yetu ni ya kinadharia na kufikirika sana. Mwalimu anamfundisha mtoto atom au cell kitu ambacho kimsingi hata ule mfano wa hicho kitu halisia hajawahi kukiona. Mara unamfundisha mapigo manne ya injini, umewahi kujiuliza ni nini kinakua kinaendelea kwenye vichwa vya wanafunzi wakati wa hizo topic? Kisha unategemea upate wataalam wanaoelewa vizuri.

Tukubali kubaki na mambo machache tukayafanya vizuri na kuelekeza nguvu kazi zetu huko, nna imani matunda yataonekana.
Tukiwa na wahitimu wa darasa la saba weney uelewa mzuri juu ya kilimo naufugaji, hali kadhalika wahitimu wa kidato cha nne na sita hadi vyuo, tutakuwa na vijana wanaotamani kuona wanaitumia elimu yao kwa vitendo zaidi ukizingatia ardhi tunayo ya kutosha. sitategemea nchi yetu kuendelea kuombaomba misaada ya chakula wakati tuna kila kitu.
 
Nasoma nije niwe mbunge au waziri hivyo ndivyo watoto wa siku hizi husemaga
 
nasoma ili nije kuajiri wasomi waniendelezee biashara yangu.
 
Back
Top Bottom